-
Somalia yajiunga na Afreximbank ili kukuza biashara ya ndani ya Afrika
Mar 25, 2025 03:14Kuanzia jana Jumatatu, Somalia imekuwa rasmi mwanachama wa 53 wa Benki ya Mauzo ya Nje ya Afrika (Afreximbank) wakati huu ambapo nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika imo kwenye jitihada za kukuza biashara ya ndani ya Afrika na uchumi wake.
-
Angola yajiondoa kama mpatanishi wa mgogoro wa DRC
Mar 25, 2025 02:41Angola imejiondoa kama mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Balozi wa A/Kusini arejea nyumbani kutoka US kwa ufakhari mkubwa
Mar 24, 2025 07:23Balozi wa Afrika Kusini ambaye rais wa Marekani Donald Trump ametaka aondoke nchini humo kutokana na kukosoa sera zake, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe.
-
Licha ya hali mbaya ya kiusalama Somalia, lakini Wasudan wakimbilia nchini humo
Mar 24, 2025 07:22Licha ya kwamba usalama nchini Somalia ni mdogo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya genge la kigaidi la al Shabab, lakini hatari nchini Sudan ni kubwa zaidi kiasi kwamba, wananchi wa Sudan wanaamua kukimbilia Somalia kuokoa maisha yao.
-
Rwanda yakaribisha uamuzi wa waasi wa M23 kuondoka katika mji wa Walikale
Mar 24, 2025 04:35Viongozi wa Rwanda wamekaribisha hatua ya waasi wa M23 ya kuondoka katika mji wa kistratejia na wenye utajiri wa madini wa Walikale na kukaribisha pia juhudi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo za kusitisha uhasama katika mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
-
Serikali ya Burkina Faso yakadhibisha kuhusu video bandia za mauaji zilizorushwa mtandaoni
Mar 24, 2025 04:31Serikali ya Burkina Faso imelaani kuenea kwa video za upotoshaji kuhusu kujiri mauaji ya umati ya kikabila nchini humo. Serikali ya Burkina Faso imesema kuwa video hizo zilizosambaa mitandaoni ni kampeni kubwa ya vyombo vya habari ya kisiasa yenye lengo la kuchafua taswira ya nchi hiyo.
-
Namibia yawa nchi ya kwanza Afrika kuwa na Rais na Makamu wa Rais mwanamke
Mar 24, 2025 00:10Rais mpya wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah ametangaza Baraza lake la Mawaziri la kwanza na kumteua Lucia Witbooi kuwa Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke wa taifa hilo.
-
Al-Shabaab waua askari polisi sita wa Kenya, wajeruhi wanne katika shambulio la alfajiri Garissa
Mar 24, 2025 00:09Askari sita wa jeshi la Polisi la Kenya wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulio linaloaminika kufanywa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab la Somalia katika kambi ya polisi iliyoko kwenye kaunti ya Garissa mashariki mwa nchi hiyo, kwenye mpaka wa pamoja na Somalia.
-
Tunisia yajitoa kwenye Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ya Umoja wa Afrika
Mar 23, 2025 23:01Tunisia imetangaza kujitoa katika Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ya Umoja wa Afrika (AfCHPR), jambo linaloashiria kupuuza serikali ya Tunis masuala ya haki na kesi zinazoendeshwa katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.
-
RSF yaua raia 45 Al-Malha; jeshi la Sudan lasonga mbele
Mar 23, 2025 07:25Zaidi ya raia 45 wameuawa katika shambulio la Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika eneo la Al-Malha, yapata kilomita 210 kaskazini mwa El Fasher, magharibi mwa Sudan.