Misri yapinga madai ya Marekani kuhusu Ukanda wa Gaza
Jumuiya ya Wahandishi wa Misri imepinga madai ya Marekani kuhusu Ukanda wa Gaza
Jumuiya hiyo imetangaza kuwa mpango ya ujenzi mpya wa haraka wa Ukanda wa Gaza unahitaji muda wa miezi sita na katika mpango huo haijaelezwa kwamba wakazi wa ukanda huo wahamishiwe sehemu nyingine.
Jumuiya ya Wahandisi wa Misri imepinga madai yaliyotolewa kwamba ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza hauwezekani bila ya kuwahamisha wakazi wa eneo hilo na imetangaza kuwa madai hayo yanatia shaka na yanatolewa lengo likiwa ni kukalia ardhi ya Gaza.
Kwa mujibu wa mpango wa Misri, wakazi wa Ukanda wa Gaza watapatiwa makazi ya muda katika maeneo maalumu kama vile shule na hospitali, na watapatiwa mahitaji yao ya kila siku hadi eneo hilo litakapojengwa upya.
Kila eneo litakalotengwa kwa ajili ya makazi ya Wapalestina litakuwa na vifaa vya kuzalisha umeme na huduma za maji.
Mpango wa ujenzi mpya wa haraka wa Ukanda wa Gaza wa Misri unaeleza kuwa: Gharama ya utekelezaji wake itafikia dola bilioni sita na kwamba vitongoji 30 vya makazi vinapaswa kutayarishwa kwa ajili ya makazi ya muda ya watu 750,000.
Hii ni katika hali ambayo, Rais Donald Trump awali alidai kuwa Wapalestina hawawezi kusalia Ukanda wa Gaza na kwamba wanapasa kuondoka katika eneo hilo.