Watu kadhaa wajeruhiwa katika maandamano ya kulalamikia kuaga dunia wanafunzi 3 Tunisia
(last modified Thu, 17 Apr 2025 13:49:24 GMT )
Apr 17, 2025 13:49 UTC
  • Watu kadhaa wajeruhiwa katika maandamano ya kulalamikia kuaga dunia wanafunzi 3 Tunisia

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika katika mji wa Mezzouna katikati mwa Tunisia kufuatia vifo vya wanafunzi watatu. Wanafunzo hao wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa shule.

Askari usalama wa Tunisia leo Alkhamisi wametumia gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji ambao jana walikusanyika ili kulalamikia hatua ya serikali ya kuutelekeza mji huo. 

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika maandamano hayo wakiwemo wawili ambao walifikishwa hopistali katika mji wa karibu wa Sfax kwa ajili ya matibabu. 

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni maandamano yameshuhudiwa katika mji wa Mezzouna katika jimbo la Sid Bouzid baada ya ukuta wa shule kuporomoka na kuuwa wanafunzi watatu. Waandamanaji wameituhumu serikali kuwa imeutelekeza mji huo. 

Walid al Jadd mwanaharakati wa Tunisia ameeleza kuwa, waandamanaji na wanachama wa asasi za kiraia wanatoa wito kwa serikali kutoa huduma za kijamii na kiuchumi kwa uadilifu ili kufufua jiji hilo,”

Rais Kais Saeid wa Tunisia ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia vifo vya wanafunzi hao watatu walioangukiwa na ukuta wa shule na ameahidi kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria wahusika wote.