-
Polisi 10 wauawa katika shambulio kwenye kituo cha polisi Niger
Jan 27, 2026 23:01Askari polisi wasiopungua 10 wa Niger wameuawa wakati watu wenye silaha waliposhambulia kituo cha polisi kaskazini mwa nchi hiyo. Eneo la kaskazini mwa Niger limekumbwa na machafuko ya magenge ya wahalifu wenye silaha.
-
Uganda inapanga kuwaondoa wanajeshi wake katika kikosi cha kulinda amani Somalia
Jan 27, 2026 10:06Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema nchi yake inapanga kuondoa wanajeshi wake huko Somalia baada ya kuwepo huko kwa kipindi cha miaka 19.
-
Waziri wa Afya wa Sudan: Watu 33,000 wameuawa katika vita vya ndani
Jan 27, 2026 08:19Waziri wa Afya wa Sudan, Dkt. Haitham Mohamed Ibrahim, ameeleza hali ya kiafya nchini Sudan baada ya miaka mitatu ya vita, akisisitiza kuwa hali imeboreka kiasi katika baadhi ya majimbo ikilinganishwa na changamoto kubwa zinazoendelea kushuhudiwa magharibi mwa Sudan na Kordofan.
-
Mali: Mashambulizi ya anga ya jeshi yameua magaidi zaidi ya 100 katika msitu wa Soussan
Jan 27, 2026 03:08Jeshi la Mali (FAMa) limetangaza kuwa limewaua zaidi ya magaidi 100 katika mashambulizi ya anga liliyofanya kwenye eneo la msitu katikati mwa nchi siku ya Jumapili, na kuyataja mashambulio hayo kuwa ni operesheni muhimu dhidi ya magaidi katika eneo hilo.
-
Makumi ya watu wauawa DRC na magaidi wenye mfungamano na ISIS
Jan 26, 2026 23:23Wanamgambo wanaohusishwa na kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) wamewaua raia wasiopungua 22 katika kijiji kimoja katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na viongozi wa asasi za kiraia.
-
Rwanda yakiri kushirikiana na waasi wa AFC/M23
Jan 26, 2026 23:04Rwanda imekiri kwa mara ya kwanza kwamba, inashirikiana na kundi la waasi wa AFC/M23 katika harakati za kiusalama huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Algeria yaijia juu Ufaransa kwa kueneza 'urongo' kupitia TV
Jan 26, 2026 07:22Serikali ya Algeria imeishutumu Ufaransa kwa kuidhinisha 'uchokozi' dhidi ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, baada ya televisheni ya serikali ya Paris kurusha makala ya matukio ya kweli (documentary) ambayo Algiers imesema imejaa "urongo na uzushi."
-
Wahamiaji 50 wahofiwa kufa maji katika ajali ya boti pwani ya Tunisia
Jan 26, 2026 06:42Serikali ya Tunisia imesema kuwa, takriban wahamiaji 50 aghalabu yao kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika wanahofiwa kufariki dunia baada ya mashua yao kupinduka katika pwani ya Tunisia.
-
Jeshi la Mali lafanya mashambulizi ya anga dhidi ya makundi ya kigaidi kusini magharibi mwa nchi
Jan 26, 2026 03:14Jeshi la Mali (FAMa) limeeleza kuwa liimefanya mashambulizi ya anga dhidi ya makundi ya kigaidi kusini-magharibi mwa nchi hiyo, na kulenga "harakati kubwa" ya wanamgambo karibu na eneo la Mourdiah.
-
Makaburi ya umati ya Khartoum yafichua sura ya giza katika vita vya Sudan
Jan 26, 2026 03:08Makaburi mawili ya umati yenye mabaki ya miili ya maelfu ya watu yalipatikana hivi majuzi mjini Khartoum mji mkuu wa Sudan. Kupatikana kwa makaburi hayo kumefichua sura ya giza katika mzozo unaoendelea Sudan kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa kundi la Rapid Support Forces (RSF)