-
Katika mazungumzo na US, Misri yahimiza Israel iondoke Ghaza, ifungue tena kivuko cha Rafah
Jan 26, 2026 00:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty ametoa wito kwa utawala wa kizayuni wa Israel kujiondoa katika Ukanda wa Ghaza na kufungua tena kivuko cha mpakani cha Rafah kuliingana na makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutekelezwa Oktoba mwaka jana.
-
Mwendesha Mashtaka wa Sudan: Tumewafungulia kesi mamluki 122 wa kigeni
Jan 25, 2026 08:14Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Sudan ameeleza kuwa kesi za jinai zimefunguliwa dhidi ya takriban mamluki 122 wa kigeni wanaopigana bega kwa bega na wanamgambo waasi wa Rapid Support Forces (RSF), huku watoto 135 waliosajiliwa kama wapiganaji katika vita hivyo wakirejeshwa kwa familia zao.
-
Mashambulizi ya mabomu ya mapipa yalazimisha watu wengi kuhama makazi yao Sudan Kusini
Jan 25, 2026 08:06Mapigano mapya nchini Sudan Kusini yamewalazimisha watu zaidi ya 180,000 kuyahama makazi yao, huku mashuhuda wakizungumzia utumiaji holela wa mabomu ya mapipa na raia kukimbilia kwenye vinamasi, huku hali tete ya ukosefu wa amani ikitanda nchini humo.
-
Mkuu wa jeshi la Sudan Kusini awapa wanajeshi siku saba kumaliza uasi
Jan 25, 2026 00:41Mkuu wa majeshi ya Sudan Kusini amewapa wanajeshi muda wa siku saba “kuukandamiza uasi” mashariki mwa nchi, ambao unatishia usalama wa mji mkuu, Juba.
-
Pande za kisiasa Sudan kuunda muungano mpya ili kurejesha utawala wa kiraia
Jan 24, 2026 09:34Makundi ya kisiasa ya Sudan ambayo yamejitenga na muungano mkuu wa demokrasia yamesema kuwa yanafanya juhudi za kuunda muungano mpana unaolenga kurejesha utawala wa kiraia nchini humo baada ya karibu miaka minne ya serikali inayoongozwa na jeshi.
-
Serikali ya Msumbiji yaomba msaada wa haraka wa kimataifa kufuatia mafuriko makubwa
Jan 24, 2026 04:24Serikali ya Msumbiji imeomba Ijumaa kwamba jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za dharura za kibinadamu ili kukabiliana na mafuriko makubwa ambayo yamesababisha maelfu kwa maelfu kuyahama makazi yao na kuharibu miundombinu katika taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Afrika.
-
DA yakanusha madai ya Trump ya kuwepo mauaji ya Wazungu A/Kusini
Jan 23, 2026 23:18Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance cha Afrika Kusini (DA), John Steenhuisen amekadhibisha madai ya kuwepo "mauaji ya kimbari ya Wazungu" nchini Afrika Kusini.
-
Afrika Kusini kujiondoa katika kundi la G20 wakati wa urais wa Marekani
Jan 23, 2026 09:11Waziri wa fedha wa Afrika Kusini, Enoch Godongwana, amethibitisha kwamba nchi hiyo itaachana na ushirikiano wake na kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi duniani G20 wakati wa urais wa Marekani katika kundi hilo.
-
Kainerugaba : Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Uganda zamesababisha vifo vya watu 30
Jan 23, 2026 08:47Mkuu wa Jeshi la Uganda na mwana wa Rais aliyechaguliwa tena, Yoweri Museveni, amesema leo Ijumaa kwamba wafuasi 30 wa upinzani wameuawa na 2,000 wamekamatwa kufuatia uchaguzi wa karibuni nchini humo.
-
Umoja wa Afrika waiondolea vikwazo Guinea
Jan 23, 2026 04:06Umoja wa Afrika umetangaza kuiondolea vikwazo Guinea ilivyoiwekea kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021, baada ya nchi hiyo kuandaa uchaguzi wa rais mwezi Disemba.