Wanamgambo wenye mfungamano na RSF wauwa raia 27 Kordofan Kaskazini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i138730-wanamgambo_wenye_mfungamano_na_rsf_wauwa_raia_27_kordofan_kaskazini
Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa wanamgambo wenye mfungamano na Kikosi cha wapiganaji wa RSF kimewaua takriban raia 27, wakiwemo wazee, katika mashambulizi dhidi ya vijiji kadhaa magharibi mwa Bara katika jimbo la Kordofan Kaskazini.
(last modified 2026-05-30T03:23:01+00:00 )
May 30, 2026 03:19 UTC
  • RSF na washirika wao wauwa raia 27 katika jimbo la Kordofan Kaskazini
    RSF na washirika wao wauwa raia 27 katika jimbo la Kordofan Kaskazini

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa wanamgambo wenye mfungamano na Kikosi cha wapiganaji wa RSF kimewaua takriban raia 27, wakiwemo wazee, katika mashambulizi dhidi ya vijiji kadhaa magharibi mwa Bara katika jimbo la Kordofan Kaskazini.

Taasisi hiyo ya tiba yenye makao yake Cairo imeeleza kuwa mashambulizi hayo yalifanywa siku ya Alhamisi katika eneo la al-Murrah, na kuyataja kama "jinai mpya inayolenga raia wasio na silaha katika maeneo ambayo ulinzi wa jeshi.

Sudan imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Aprili 2023, wakati mvutano wa muda mrefu kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF ulipozuka na kuwa mzozo mkubwa ambao umeua mamia kwa maelfu ya watu na kupelekea mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Eneo la Kordofan limekuwa mojawapo ya viwanja vikuu vya vita, huku mapigano yakishtadi katika pande kadhaa, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

RSF na wapiganaji waitifaki wao wanadhibiti sehemu kubwa ya eneo la magharibi la Darfur, pamoja na baadhi ya maeneo ya Kordofan katika mpaka na Sudan Kusini, maeneo yenye utajiri wa mafuta na migodi ya dhahabu.