-
Rais mpya wa Ghana ateuwa mawaziri wake wa awali
Jan 10, 2025 23:26Rais mpya wa Ghana, John Dramani Mahama, ameweka wazi uteuzi wake muhimu katika baraza la mawaziri la serikali ijayo ya nchi hiyo kwa kuwateuwa Cassiel Ato Forson kuwa Waziri wa Fedha, John Abdulai Jinapor Waziri wa Nishati, na Dominic Akuritinga Ayine kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria.
-
Rais Ouattara aonyesha kiu ya kuwania tena urais wa Ivory Coast kwa muhula wa nne mfululizo
Jan 10, 2025 06:52Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amesema, angependa kuendelea kusalia madarakani licha ya chama chake kutopitisha hadi sasa jina la mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa urais utakaofanyika baadaye mwaka huu.
-
Wapakistan wanane wapandishwa kizimbani Tanzania kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya
Jan 10, 2025 03:30Raia wanane wa Pakistan wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam Tanzania wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kusafirisha madawa ya kulevya.
-
Kinara wa upinzani nchini Msumbiji arejea kutoka uhamishoni
Jan 09, 2025 23:08Kinara wa upinzani nchini Msumbiji Venancio Mondlane jana alirejea nchini kutoka uhamishoni wakati vikosi vya usalama vikifyatua mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia ya wafuasi wake.
-
Rais Kagame akanusha madai dhidi ya nchi yake ya kuunga mkono waasi wa M23
Jan 09, 2025 23:07Rais Paul Kagame wa Rwanda, kwa mara nyingine tena amekanusha madai dhidi ya ya nchi yake ya kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
-
Walibya wakasirishwa na hatua za kutaka kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Israel
Jan 09, 2025 22:57Kufichuliwa maelezo ya kina zaidi ya kikao cha Waziri wa zamani wa Mashauri ya Kigeni ya Libya na mwenzake wa utawala wa Kizayuni wa Israel kumeibua wimbi la maandamano nchini Libya.
-
Rais Ruto afanya mazungumzo na rais wa Angola João Lourenço
Jan 09, 2025 09:00Rais wa Kenya, William Ruto, amekamilisha ziara fupi nchini Angola, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo mjini Luanda na Rais João Lourenço wa nchi hiyo.
-
Watu 19 wauawa Chad katika shambulio dhidi ya Ikulu ya Rais
Jan 09, 2025 07:22Watu wenye silaha wameshambulia Ikulu ya Rais nchini Chad katika mji mkuu N’Djamena, na kuzua mapigano ambayo yameua washambuliaji 18 na afisa mmoja wa usalama na wengine kadhaa kujeruhiwa.
-
Wananchi wa Morocco wakusanyika mbele ya jengo la Bunge kulaani jinai za Israel
Jan 09, 2025 07:21Wananchi wa Morocco wameandamana na kukusanyika mbele ya jengo la bunge la nchi hiyo mjini Rabat kuonyesha uungaji mkono wao kwa Palestina na kupinga mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
IGP wa Kenya hatarini kushtakiwa na kuhukumiwa baada ya kudharau mara 2 wito wa kufika mahakamani
Jan 09, 2025 02:40Mahakama nchini Kenya imetishia kumhukumu Inspekta Jenerali wa Polisi wa nchi hiyo iwapo hatafika mahakamani kwa tarehe itakayopangwa.