-
Somaliland na Ethiopia zakubaliana kutatua kwa amani mzozo unaoendelea
Dec 27, 2024 07:17Maafisa kutoka Jamhuri iliyojitangazia uhuru wake ya Somaliland na wenzao wa Ethiopia wamekubaliana kutatua kwa amani mapigano makali ambayo yametokea katika kipindi cha wiki tatu zilizopita katika kijiji cha mpakani cha Da'awaley.
-
Polisi ya Kenya 'yasutwa' kwa kudai hakuna Wakenya waliotekwa nyara
Dec 27, 2024 03:54Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) imekanusha ripoti ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kwamba hakuna Wakenya waliotekwa nyara nchini humo ikisema, katika mwezi huu wa Desemba pekee, watu saba hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii wametekwa nyara; na kufikia sasa, sita hawajulikani waliko.
-
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 'ladungua ndege zisizo na rubani' za Rwanda
Dec 26, 2024 23:28Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo limeatangaza kuwa, 'limedungua' ndege sita zisizo na rubani za Kamikaze za jeshi la Rwanda katika mji wa Mambasa eneo la Lubero katika Mkoa wa Kivu Kaskazini.
-
Ethiopia 'yafunga mpaka na Somaliland' baada ya mapigano ya kikabila kuua zaidi ya watu 100
Dec 26, 2024 23:26Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa, imefunga mpaka wake na Jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland baada ya siku kadhaa za mapigano yaliyoigharimu pakubwa roho za watu katika maeneo ya mpakani ambayo yamezua mvutano na Hargeisa.
-
Uasi ndani ya jela Msumbiji, wafungwa 33 wauawa, zaidi ya 1,500 watoroka
Dec 26, 2024 07:00Wafungwa wasiopungua 1,534 wametoroka katika jela moja iliyoko karibu na mji mkuu wa Msumbiji, Maputo katika tukio linalodaiwa kupangwa na kuhusishwa na maandamano ya machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba.
-
Rais Ruto wa Kenya: Vijana wajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya na mihadarati
Dec 26, 2024 03:19Rais William Ruto wa Kenya amewataka vijana wajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya na mihadarati.
-
Maelfu wakimbia vita Sudan, warundikana kwenye mpaka wa Sudan Kusini
Dec 25, 2024 08:45Vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan vimesababisha zaidi ya watu 80,000 kukimbilia Sudan Kusini katika muda wa chini ya wiki tatu. Wengi wao wamekwama mpakani.
-
Wapinzani Chad wataka kususiwa uchaguzi, wadai si wa kidemokrasia
Dec 25, 2024 08:44Wakati uchaguzi wa wabunge na serikali za mitaa nchni nchini Chad ambao umepangwa kufanyika Disemba 29 unapozidi kukaribia, mjadala mkali unaendelea katika mitaa ya mji mkuu N'Djamena.
-
WHO yaonya juu ya ongezeko la kutisha la kesi za malaria nchini Ethiopia
Dec 25, 2024 08:44Ethiopia imeripoti kesi milioni 8.4 za ugonjwa wa malaria tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
-
Ukatili wa kijinsia unazidi kuongezeka Kenya, matukio zaidi ya 7,000 yameripotiwa katika mwaka mmoja
Dec 25, 2024 03:24Kenya inakabiliwa na ongezeko la kutisha la ukatili wa kijinsia, baada ya kesi zaidi ya 7,100 kuripotiwa tangu Septemba 2023, ikiwa ni pamoja na mauaji 100 yaliyorekodiwa ya wanawake tangu Agosti mwaka huu. Hayo ni kwa mujibu wa rekodi za serikali.