-
Wakuu wa Intelijinsia wa Ethiopia na Somalia wakutana huku nchi mbili zikiendelea kuimarisha uhusiano
Dec 24, 2024 22:49Redwan Hussein Mkuu wa Intelijinsia wa Ethiopia jana Jumanne alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Somalia Abdullahi Mohamed Ali huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia ili kuendeleza ushirikiano wa kiusalama na kuimarisha ahadi zilizoainishwa katika Azimio la Ankara.
-
Rais wa Nigeria apongeza mpango wa nchi hiyo wa mabadiliko ya kodi
Dec 24, 2024 22:48Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema kuwa atasonga mbele na miswada minne ya marekebisho ya kodi ambayo tayari imewasilishwa bungeni licha ya kukabiliwa na radiamali hasi ya magavana kadhaa wa majimbo nchini humo.
-
Baraza la Katiba la Msumbiji lamtangaza Daniel Chapo kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais
Dec 24, 2024 03:20Baraza la Katiba la Msumbiji (CC) ambacho ni chombo kinachosimamia masuala ya katiba na uchaguzi nchini humo, jana Jumatatu lilimtangaza Daniel Chapo kuwa mshindi wa urais wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 9.
-
Al Burhan autaka Umoja wa Mataifa kuzuia kumiminwa silaha huko Darfur Sudan
Dec 24, 2024 03:19Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba maazimio ya Baraza la Usalama ya kuzuia kuingizwa silaha katika eneo la Darfur la magharibi mwa Sudan na mashambulizi katika mji wa El Fasher yanaheshimiwa kikamilifu.
-
Mwendesha Mashtaka wa Umma Sudan aahidi kuwafungulia mashtaki makamanda wa RSF
Dec 23, 2024 23:56Mwendesha Mashtaka wa Umma nchini Sudan, Al-Fatih Mohamed Issa Tayfour, ameahidi kuwafungulia mashtaka wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mahakama za kitaifa.
-
Wananchi wa Sudan Kusini wanataabika na mafuriko
Dec 23, 2024 23:02Mafuriko ya msimu yaliyoiathiri Sudan Kusini, ambayo hapo huko nyuma yalikuwa yanatabirika na yalikuwa ni sehemu ya maisha ya watu wa maeneo hayo, sasa yamekuwa janga la kila mwaka, na kuwalazimisha mamia ya maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
-
Kimbunga Chido kinazidi kuteketeza roho za watu huko Msumbiji; Watu 94 wameaga dunia
Dec 23, 2024 10:45Taasisi ya Taifa ya Kushughulikia Majanga ya Kimaumbile ya Msumbiji (INGD) imetangaza kuwa kimbunga Chido hadi sasa kimeuwa watu 94 nchini humo tangu kilipoiathiri nchi hiyo wiki iliyopita.
-
Mamia ya wafungwa waachiliwa huru katika gereza la Makala DRC
Dec 22, 2024 23:41Mamia ya wafungwa wameachiliwa huru kutoka katikak gereza la makala katuika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Rais wa Ufaransa akiri, Afrika imebadilika
Dec 22, 2024 08:48Wakati Ufaransa imepoteza kambi zake nyingi za kijeshi barani Afrika, sasa rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron, katika safari ya kimyakimya kwenye kituo cha mwisho cha operesheni za nchi hiyo huko Djibouti, amekiri kwamba: Afrika inabadilika kwa sababu maoni ya umma na Serikali yamo katika hali ya kubadilika, hivyo nafasi yetu barani Afrika pia itabadilika.
-
Nigeria yakanusha madai ya kula njama ya kuyumbisha amani huko Niger
Dec 22, 2024 04:32Nigeria imekanusha "kwa matamshi makali sana" tuhuma za Niger kwamba inapanga njama ya kuyumbisha nchi hiyo kwa kuwasaidia wanamgambo waliofanya mashambulizi kwenye bomba muhimu la mafuta la nchi hiyo.