Mamia ya wafungwa waachiliwa huru katika gereza la Makala DRC
Mamia ya wafungwa wameachiliwa huru kutoka katikak gereza la makala katuika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mamlaka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema imewaachilia huru wafungwa 600 katika gereza kuu la nchi hiyo la Makala kama sehemu ya mpango wa kupunguza msongamano katika magereza ya nchi hiyo.
Waziri wa sheria, Constant Mutamba ametangaza hatua hiyo wakati wa sherehe katika gereza hilo la Makala katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasha huku akiongeza kwamba serikali ya nchi hiyo ipo katika mipango ya ujenzi wa gereza jipya huko Kinshasa.
Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ilionyesha kwamba gereza la Makala ambalo ndio gereza kubwa zaidi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lina uwezo wa kuchukua watu 1,500 lakini linawashikilia zaidi ya wafungwa 12,000, wengi wao wakiwa bado wanasubiri kesi zao kusikilizwa.
Mwezi Septemba mwaka huu kkwa akali watu 129 walithibitishwa kuuawa na wengine 59 kujeruhiwa wakati wa jaribio la kutoroka jela katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wafungwa wengine waliaga dunia kutokana na mkanyagano au kukosa hewa.
Ikumbukwe kuwa, wanamgambo wenye silaha wamekuwa wakivamia magereza na jela za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuachilia huru mamia ya wafungwa.