Jeshi la Israel lawanyanyasa kingono wanaharakati wa Al-Samoud Global Flotilla
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138242-jeshi_la_israel_lawanyanyasa_kingono_wanaharakati_wa_al_samoud_global_flotilla
Wakati mjadala wa mzingiro wa Ukanda wa Gaza na kampeni za kimataifa za kuvunja mzingiro huo wa utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo ukiendelea, kundi la Al-Samoud Global Flotilla, limechapisha ushuhuda kutoka kwa wanaharakati wake walioachiliwa huru, likishutumu jeshi la Israel kuwa limewanyanyasa kimwili na kingono washiriki wa msafara huo.
(last modified 2026-05-09T08:06:34+00:00 )
May 09, 2026 07:59 UTC
  • Al-Samoud Global Flotilla
    Al-Samoud Global Flotilla

Wakati mjadala wa mzingiro wa Ukanda wa Gaza na kampeni za kimataifa za kuvunja mzingiro huo wa utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo ukiendelea, kundi la Al-Samoud Global Flotilla, limechapisha ushuhuda kutoka kwa wanaharakati wake walioachiliwa huru, likishutumu jeshi la Israel kuwa limewanyanyasa kimwili na kingono washiriki wa msafara huo.

Al-Samoud Global Flotilla imetangaza kwamba askari wa Israel waliwabaka na kuwadhalilidha kingono" wanaharakati kadhaa waliokuwepo kwenye msafara huo uliokuwa na misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza baada ya kukamata meli zao katika maji ya kimataifa karibu ya pwani ya Ugiriki.

Taarifa iliyotolewa na Al-Samoud Global Flotilla imesema kwamba uongozi wa msafara huo umepokea "ushahidi wa kimsingi na wa moja kwa moja" ambao ulionyesha "mtindo wa utaratibu wa kupanga wa unyanyasaji mkali wa kimwili, wa kingono na udhalilishaji wa makusudi" dhidi ya washiriki katika msafara huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ushahidi huo ulikusanywa baada ya wanachama 179 wa flotilla kuachiliwa na kukabidhiwa kwa mamlaka ya Ugiriki.

Kwa uchache wanaharakati wanne waliripotiwa kufanyiwa ukatili wa kingono na wanajeshi wa Israel.

Meli hizo ni sehemu ya msafara wa pili wa Global Sumud ambao katika miezi ya karibuni umekuwa ukijaribu kuvunja mzingiro wa Israel kwa kusafirisha misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina huko Gaza. Msafara huo uliondoka katika bandari ya Barcelona, Hispania, tarehe 12 Aprili.

Meli hizo zilikamatwa karibu na rasi ya Peloponnese nchini Ugiriki, mamia ya maili kutoka Gaza.

Katika taarifa yake, msafara wa Sumud umesema wanaharakati 31 walijeruhiwa wakati wa shambulio la vikosi vya Israel.