Rais wa Nigeria apongeza mpango wa nchi hiyo wa mabadiliko ya kodi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120560-rais_wa_nigeria_apongeza_mpango_wa_nchi_hiyo_wa_mabadiliko_ya_kodi
Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema kuwa atasonga mbele na miswada minne ya marekebisho ya kodi ambayo tayari imewasilishwa bungeni licha ya kukabiliwa na radiamali hasi ya magavana kadhaa wa majimbo nchini humo.
(last modified 2025-10-17T12:36:14+00:00 )
Dec 25, 2024 02:18 UTC
  • Rais wa Nigeria apongeza mpango wa nchi hiyo wa mabadiliko ya kodi

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema kuwa atasonga mbele na miswada minne ya marekebisho ya kodi ambayo tayari imewasilishwa bungeni licha ya kukabiliwa na radiamali hasi ya magavana kadhaa wa majimbo nchini humo.

Wachambuzi wamambo wanasema kuwa mabadiliko haya ni sehemu ya jitihada za Rais wa Nigeria za kurekebisha mfumo wa kodi ili kuingiza mapato zaidi katika uchumi wa nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo pendekezo la jinsi ya kugawana Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT) kati ya serikali kuu na majimbo 36 ya Nigeria  limezua mzozo, huku sehemu ya wabunge wa shirikisho wakidai kuwa itapunguza mgao kwa eneo la kaskazini mwa nchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wiki hii, Rais Bola Tinubu wa Nigeria amesema: " Mabadiliko ya kodi yako pale pale. Hatuwezi kuendelea kufanya mambo kwa mazoea katika uchumi wa dunia ya leo kama tulivyokuwa tukifanya kwa miaka kadhaa sasa". 

Mwezi jana bunge la Nigeria lilianza kujadili miswada minne ambayo Rais wa nchi hiyo ameitaja kuwa ni "Mapambazuko Mapya."