-
Watu 2,460 wameshapoteza maisha katika ajali za barabarani nchini Libya mwaka 2024
Dec 22, 2024 00:09Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali za barabarani nchini Libya tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024 hadi hivi sasa imeshafikia 2,460. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi na Faisal Barnus, Mkuu wa Idara ya Uusafiri wa Barabarani na Leseni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya.
-
Watu zaidi ya 20 wapoteza maisha katika mkanyagano wakati wa ugawaji wa chakula huko Nigeria
Dec 21, 2024 10:31Takriban watu 20 wamepoteza maisha katika tukio la mkanyagano lililotokea katika zoezi la ugawaji chakula katika Jimbo la Anambra, kusini mashariki mwa Nigeria.
-
Serikali ya Kenya kufuatilia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofadhili ugaidi
Dec 21, 2024 09:28Serikali ya Kenya imetangaza kuuwa, inayafuatilia mashirika yasiyo ya serikali yanayotumia vibaya fedha za wafadhili kusaidia shughuli haramu ikiwemo ugaidi.
-
UNICEF: Tuna wasiwasi na hatima ya watoto walio katika mazingira magumu Msumbiji
Dec 21, 2024 09:27Serikali ya Msumbiji jana ilitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa karibu wiki moja baada ya Kimbunga Chido kupiga baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Kulingana na ripoti ya awali, watu 73 waliuawa na wengine 600 kujeruhiwa.
-
Rais Tshisekedi afanya mabadiliko makubwa katika jeshi la DRC
Dec 21, 2024 09:26Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amemfuta kazi mkuu wa majeshi na maafisa wengine wa ngazi ya juu katika jeshi la taifa, katika mabadiliko makubwa ndani ya jeshi wakati mapigano makali yanaendelea kati ya jeshi la serikali na waasi mashariki mwa nchhi hiyo.
-
Wanajeshi wa Ufaransa waanza kuondoka Chad
Dec 21, 2024 03:38Kikosi cha wanajeshi 120 wa Ufaransa kimeondoka Chad kufuatia uamuzi wa nchi hiyo kusitisha mkataba wake wa ushirikiano wa kiulinzi na Paris.
-
Malawi inadai mabilioni ya dola kutoka kwa kampuni ya madini ya Marekani
Dec 21, 2024 03:37Serikali ya Malawi inadai dola bilioni 309 za kodi na mrabaha ambazo hazijalipwa kutoka kwa kampuni ya Marekani ya Columbia Gem House kwa ajili ya mawe ya thamani yaliyouzwa nje katika muongo mmoja uliopita.
-
MONUSCO kuendelea kubakia DRC baada ya kongezewa muda
Dec 21, 2024 03:36Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuongeza muda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC (MONUSCO), hadi tarehe 20 Desemba 2025.
-
Hofu yatanda Msumbiji kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi
Dec 20, 2024 23:27Msumbiji inajiandaa kwa maandamano zaidi huku matokeo ya mwisho ya uchaguzi unaodaiwa na wapinzani kuwa ulikuwa na utata yakitarajiwa kutangaza kabla yya Jumatatu ijayo.
-
Zaidi ya watu 10,000 waambukizwa ugonjwa wa rubella Afrika Kusini
Dec 20, 2024 10:00Idara ya Afya ya Afrika Kusini imewatahadharisha wananchi kuhusu ongezeko kubwa la wagonjwa wa rubella kote nchini humo hasa kutokana na kuripotiwa zaidi ya kesi 10,000 za watu walioambukizwa ugonjwa huo mwaka huu.