Wanajeshi wa Ufaransa waanza kuondoka Chad
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120416-wanajeshi_wa_ufaransa_waanza_kuondoka_chad
Kikosi cha wanajeshi 120 wa Ufaransa kimeondoka Chad kufuatia uamuzi wa nchi hiyo kusitisha mkataba wake wa ushirikiano wa kiulinzi na Paris.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Dec 21, 2024 03:38 UTC
  • Wanajeshi wa Ufaransa waanza kuondoka Chad

Kikosi cha wanajeshi 120 wa Ufaransa kimeondoka Chad kufuatia uamuzi wa nchi hiyo kusitisha mkataba wake wa ushirikiano wa kiulinzi na Paris.

Wanajeshi wa Ufaransa walionekana wakipanda ndege yao siku ya Ijumaa na kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa N'Djamena.

Mchakato wa kujiondoa ulianza rasmi mapema mwezi huu kwa kuondoka kwa ndege mbili za kivita za Mirage.

Ufaransa bado ina wanajeshi wapatao 1000 walioko nchini Chad, huku uondoaji kamili ukitarajiwa kuchukua wiki kadhaa.

Masharti ya uondoaji kamili, ikiwa ni pamoja na kama wanajeshi wowote wa Ufaransa watasalia nchini Chad, bado hayajakamilika kati ya nchi hizo mbili.

Chad ilitangaza mnamo Novemba 28 uamuzi wake wa kusitisha makubaliano ya kijeshi na Paris yaliyoanza kutekelezwa baada ya nchi hiyo kujinyakulia uhuru kutoka Ufaransa mnamo 1960.

Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa Chad kumekuja baada ya Ufaransa kulazimishwa kuondoa vikosi vyake kutoka Mali, Burkina Faso, Niger na Senegal katika miaka ya hivi karibuni.

Kuondoka huku kunaashiria mwisho wa miongo kadhaa ya uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa katika eneo la Sahel huku hisia za chuki dhidi ya Ufaransa zikiendelea kukua.