CIA yakiri: Iran inaweza kuhimili mzingiro wa baharini wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138262-cia_yakiri_iran_inaweza_kuhimili_mzingiro_wa_baharini_wa_marekani
Shirika la Ujasusi la Marekani limekiri kuwa Iran ina uwezo wa kuhimili athari za mzingiro wa nchi hiyo kwa miezi kadhaa, na pia ina hifadhi kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani.
(last modified 2026-05-09T09:59:14+00:00 )
May 09, 2026 09:57 UTC
  • CIA yakiri: Iran inaweza kuhimili mzingiro wa baharini wa Marekani

Shirika la Ujasusi la Marekani limekiri kuwa Iran ina uwezo wa kuhimili athari za mzingiro wa nchi hiyo kwa miezi kadhaa, na pia ina hifadhi kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani.

CIA imetilia shaka madai ya Rais Donald Trump kwamba Tehran inataka vita vimalizike haraka iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na gazeti la The Washington Post siku ya Jumamosi, uchambuzi mpya wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) umeonyesha kuwa Iran ina uwezo mkubwa wa kustahimili kuliko ilivyodhaniwa na inaweza kuhimili ugumu wa kiuchumi kutokana na mzingiro hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Ripoti hiyo ya siri iliwasilishwa kwa maafisa wa serikali ya Trump mapema wiki hii.

Iran pia ina uwezo wa kuuza mafuta yake kupitia njia za nchi kavu kwa malori na reli, na hivyo kusaidia ustawi wa kiuchumi wa nchi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, imeelezwa kuwa upo uwezekano wa Iran kuanza kuuza mafuta yake kwa njia ya reli kupitia Asia ya Kati.