Burundi kufanya uchaguzi wa rais Mei 3 mwaka ujao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i138252-burundi_kufanya_uchaguzi_wa_rais_mei_3_mwaka_ujao
Burundi itafanya uchaguzi wa rais Mei 3 mwaka ujao. Habari hiyo ilitangazwa Ijumaa na Tume ya Uchaguzi, wakati wa mkutano uliosusiwa na upinzani.
(last modified 2026-05-09T09:49:57+00:00 )
May 09, 2026 09:47 UTC
  • Burundi kufanya uchaguzi wa rais Mei 3 mwaka ujao

Burundi itafanya uchaguzi wa rais Mei 3 mwaka ujao. Habari hiyo ilitangazwa Ijumaa na Tume ya Uchaguzi, wakati wa mkutano uliosusiwa na upinzani.

Rais Evariste Ndayishimiye ameiongoza nchi hiyo ndogo ya Afrika Mashariki yenye watu milioni 15 ambayo haina bahari, kufuatia kifo cha kiongozi aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu, Pierre Nkurunziza, mwaka 2020.

Burundi ni kati ya nchi maskini zaidi barani Afrika na kwa miaka mingi imeathiriwa na migogoro ya ndani na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wapinzani Burundi wamekuwa wakidai kukandamizwa na serikali kuu.

Ndayishimiye aliye na umri wa miaka 57, mwezi Aprili alitajwa kuwa mgombea wa chama chake tawala cha CNDD-FDD, na anatazamwa na wengi kama mgombea mwenye nafasi mkubwa ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa rais mwaka kesho.

Wapinzani Burundi wamesema katika taairfa yao ya pamoja kuwa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo haina uwezo wa kuandaa uchaguzi utakaokidhi viwango vinavyohitajika vya uwazi na haki.