Rais Tshisekedi afanya mabadiliko makubwa katika jeshi la DRC
-
Rais Felix Tshisekedi
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amemfuta kazi mkuu wa majeshi na maafisa wengine wa ngazi ya juu katika jeshi la taifa, katika mabadiliko makubwa ndani ya jeshi wakati mapigano makali yanaendelea kati ya jeshi la serikali na waasi mashariki mwa nchhi hiyo.
Katika mabadiliko hayo, mkuu wa majeshi Jenerali Christan Tshiwewe, ambaye amekuwa ofisini tangu Oktoba 2022, amefutwa kazi na nafasi yake imechukuliwa na Luteni Jenerali Jules Banza Mwilambwe.
Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Walinzi wa Jamhuri, alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa majeshi mnamo Oktoba 2022 kwa dhamira ya kukabiliana na kusonga mbele kwa M23, kundi la waasi lakini inasemekana amefutwa katika nafasi hiyo kutokana na kuendelea kuzorota usalama nchini humo.
Mabadiliko hayo yanafanyika huku serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiendelea kukabiliana na makundi ya waasi hasa mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamehatarishha usalama wa raia.
Wimbi la mashambulizi mapya ya waasi wa M23 na ADF linaendelea kuwatesa wananchi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) huku mapigano baina ya wanajeshi wa serikali na waasi wa makundi hayo mawili yakiendelea.
Genge jingine la waasi mashariki mwa DRC ni lile la waasi wa M23, ambao viongozi wa DRC wanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono. Waasi hao nao kama wale wa ADF hivi sasa wameshadidisha mashambulizi yao mashariki mwa nchi hiyo.