UNICEF: Tuna wasiwasi na hatima ya watoto walio katika mazingira magumu Msumbiji
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120424-unicef_tuna_wasiwasi_na_hatima_ya_watoto_walio_katika_mazingira_magumu_msumbiji
Serikali ya Msumbiji jana ilitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa  karibu wiki moja baada ya Kimbunga Chido kupiga baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Kulingana na ripoti ya awali, watu 73 waliuawa na wengine 600 kujeruhiwa.
(last modified 2024-12-21T09:27:46+00:00 )
Dec 21, 2024 09:27 UTC
  • UNICEF: Tuna wasiwasi na hatima ya watoto walio katika mazingira magumu Msumbiji

Serikali ya Msumbiji jana ilitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa  karibu wiki moja baada ya Kimbunga Chido kupiga baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Kulingana na ripoti ya awali, watu 73 waliuawa na wengine 600 kujeruhiwa.

Wakati zoezi la kutafuta miili na manusura bado linaendelea Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa lina wasiwasi kuhusiana na hatima ya watoto nchini humo.

Taarifa ya UNICEF imesema, kuna haja ya kuchhuukuliwa hatua za kuwalinda watoto hasa katika kipindi hiki kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na janga hilo la kimaumbile.

Kimbunga hicho, ambacho kimepiga mikoa ya Cabo Delgado na Nampula, kimesababisha uharibifu mkubwa na kulazimisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Mashirika ya kibinadamu yameanza kutoa msaada wa dharura na kutaka ufadhili wa ziada wa kusaidia takriban watu 182,000 walioathirika.

Katika upande Msumbiji inajiandaa kwa maandamano zaidi huku matokeo ya mwisho ya uchaguzi unaodaiwa na wapinzani kuwa ulikuwa na utata yakitarajiwa kutangaza kabla ya Jumatatu ijayo.

Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane ametishia kuitisha uasi wa nchi nzima kama Baraza la Katiba litaidhinisha matokeo ya awali ambayo yalimuweka katika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Oktoba 9 akishindwa na mgombea wa chama tawala cha Frelimo.

Takriban watu 90 wameuawa na wengine 340 kujeruhiwa tangu ghasia za baada ya uchaguzi kuikumba Msumbiji mwezi Oktoba mwaka huu.