-
Misri yalalamika dhidi ya Ethiopia katika Umoja wa Mataifa
Sep 03, 2024 01:03Misri imewasilisha malalamiko yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), ikiishutumu Ethiopia kwa kutishia uthabiti wa kikanda kwa hatua za upande mmoja kuhusu mradi wa kutatanisha wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) kwenye Mto Nile.
-
Wizara ya Afya: Idadi ya vifo kutokana na mafuriko Sudan imefikia watu 173
Sep 02, 2024 07:32Wizara ya Afya ya Sudan imesema katika ripoti yake ya karibuni kabisa kwamba mvua kubwa na mafuriko yaliyoikumba nchi hiyio yamesababisha vifo vya watu 173 na kujeruhi wengine 505 tangu mwanzoni wa msimu wa mvua wa mwezi Juni mwaka huu.
-
Afisa wa jeshi la Libya aliyekuwa akisakwa na Interpol auawa mjini Tripoli
Sep 02, 2024 07:32Watu waliokuwa na silaha wasiojulikana wamemuua kamanda wa kambi ya Chuo cha Jeshi la Wanamaji la Libya mjini Tripoli, Abd al-Rahman Milad, aliyepewa jina la utani la "Al-Bija," baada ya kummiminia risasi katika mjini Tripoli.
-
Shirika la Ujerumani: Hali mbaya ya hewa ndiyo iliyosababisha kifo cha Makamu wa Rais wa Malawi
Sep 02, 2024 03:45Shirika moja la Ujerumani lililokuwa linafanya uchunguzi kuhusu kifo cha Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Chilima, limesema katika ripoti yake kwamba, hali mbaya ya hewa iliyopelekea rubani kushindwa kuona vizuri, ndiyo sababu ya ajali ya ndege iliyopelekea kufariki dunia Chilima na watu wengine wanane tarehe 10 Juni mwaka huu.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan: OIC imeitambua RFS kama "kikosi cha waasi"
Sep 02, 2024 00:06Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imetangaza kwamba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imepitisha - kwa mara ya kwanza - uamuzi unaovitambua Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kama "kikosi cha waasi". Uamuzi huo rasmi uliotolewa na Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya hiyo katika kikao chake cha hamsini, ambacho ilifanyika Yaoundé, Cameroon, Agosti 29 na 30.
-
Nigeria kuanza kutoa chanjo ya Mpox kuanzia Oktoba 8
Sep 01, 2024 23:31Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, itaanza kutoa chanjo ya kukabiliana na virusi vya homa ya Mpox kuanzia Oktoba 8, baada ya uidhinishaji wa chanjo hiyo kukamilika nchini humo.
-
Museveni aunga mkono mahusiano ya vyombo vya habari kati ya China na Afrika
Sep 01, 2024 09:27Kampeni ya vyombo vya habari inayojulikana kama “Washirika wa Afrika” iliyoandaliwa na China Media Group (CMG) itakuza mahusiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika, na kuimarisha ushirikiano kwa vitendo baina yao.
-
UN yahimiza misaada zaidi kwa ajili ya Sudan, yasema iliyotolewa haijawapunguzia mateso raia
Sep 01, 2024 06:43Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed, ametoa wito wa kutolewa misaada zaidi kwa Sudan akisisitiza kwamba, juhudi zilizofanywa hadi sasa katika uga huo hazijatosha kupunguza mateso wanayopata raia wa nchi hiyo.
-
Mali: Silaha za Magharibi zinaimarisha ugaidi barani Afrika
Sep 01, 2024 03:51Mwakilishi wa Kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, sehemu kubwa ya silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kwa Ukraine zinahamishiwa katika eneo la Sahel barani Afrika na kushadidisha harakati za ugaidi barani humo.
-
Silaha za Magharibi huko Ukraine zinavuruga usalama barani Afrika
Sep 01, 2024 03:35Mwakilishi wa Kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa, Issa Konfourou, ametangaza kwamba silaha nyingi za nchi za Magharibi ambazo hutolewa kwa Ukraine zinapelekwa katika eneo la Sahel barani Afrika na kuchochea uhalifu na ugaidi.