Silaha za Magharibi huko Ukraine zinavuruga usalama barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i115882-silaha_za_magharibi_huko_ukraine_zinavuruga_usalama_barani_afrika
Mwakilishi wa Kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa, Issa Konfourou, ametangaza kwamba silaha nyingi za nchi za Magharibi ambazo hutolewa kwa Ukraine zinapelekwa katika eneo la Sahel barani Afrika na kuchochea uhalifu na ugaidi.
(last modified 2024-09-01T03:35:32+00:00 )
Sep 01, 2024 03:35 UTC
  • Silaha za Magharibi huko Ukraine zinavuruga usalama barani Afrika

Mwakilishi wa Kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa, Issa Konfourou, ametangaza kwamba silaha nyingi za nchi za Magharibi ambazo hutolewa kwa Ukraine zinapelekwa katika eneo la Sahel barani Afrika na kuchochea uhalifu na ugaidi.

Mwakilishi wa Kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba, anafanya jitihada za kuzuia kuendelea mchakato huo kwa kuangazia wasiwasi mkubwa wa nchi za eneo la Sahel Afrika kuhusu athari mbaya za kutuma silaha huko Ukraine kwa usalama wa Afrika; kwa sababu inajulikana kwamba, sehemu kubwa ya silaha za nchi za Magharibi ambazo ziko mikononi mwao Ukraine, hatimaye inatumiwa kuchochea ugaidi na uhalifu barani Afrika na maeneo mengine, jambo ambalo linazidisha hatari ya kukosekana utulivu.

Matamshi haya ya kutia wasiwasi yanayotolewa kwenye duru mbalimbali yanaonyesha kuwa, nchi za Magharibi zinafuatilia malengo kadhaa katika mgogoro wa Ukraine, muhimu zaidi ikiwa ni kusaidia ustawi wa viwanda vya silaha vya Magharibi na kuimarisha makundi ya kigaidi.

Makundi ya waasi Sahel Afrika yanapata silaha kutoka Ukraine

Ali Sharifinia, mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema: "Ukraine ni chombo tu kinachutumiwa na nchi za Magharibi, hasa Marekani, kutekeleza sera zao za kuzusha migogoro na machafuko katika maeneo mbalimbali ya dunia. Hii ina maana kwamba, Ukraine ni jukwaa la kusafirisha silaha za kisasa za Kimagharibi hadi maeneo mengine ya dunia, ikiwa ni pamoja na nchi Sahel Afrika. Madalali na wauzaji wa silaha wamekuwa na harakati kubwa zaidi, na kutokana na fursa wanazopewa na duru za Magharibi kwa ajili ya ulanguzi wa silaha kutoka Ukraine, sasa usafirishaji silaha kutoka nchini humo hadi maeneo mengine umekuwa rahisi zaidi."

Kutokana na hali hiyo, mwakilishi wa Mali katika Umoja wa Mataifa, amezitaka nchi zinazotuma silaha huko Ukraine kuhakikisha kwamba, silaha hizo hazifiki mikononi mwa magaidi na makundi yenye itikadi kali yanayofanya harakati za kihalifu barani Afrika. Kwa sababu, Mali haitaki kuwa uwanja wa vita vya wakala kati ya mataifa yenye nguvu duniani. Wasiwasi huo wa mwakilishi wa Mali kuhusu utoroshaji wa silaha za nchi za Magharibi kutoka Ukraine hadi Afrika, unastahili kupewa mazingatio kwa kutilia maanani mapinduzi mtawalia yaliyotokea barani Afrika, ikiwemo nchi ya Mali yenyewe. Ikumbukwe pia kwamba, mwezi Julai mwaka huu makundi ya waasi yalishambulia jeshi la Mali kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa kwa jeshi na serikali ya nchi hiyo. Baada ya mashambulizi hayo ya kigaidi, Mali na kisha Niger zilikata uhusiano wao wa kidiplomasia na Ukraine kutokana na msaada wa Kiev kwa makundi ya kigaidi.

Duru za vyombo vya habari nchini Marekani zinaamini kuwa, nchi za Magharibi zinajua vyema kwamba nchi zinazopakana na Ukraine zimejaa silaha zinazotumwa na nchi za Wamagharibi, hasa Marekani kuelekea Ukraine. Katika muktadha huu, mwandishi wa habari za kiuchunguzi wa Marekani, Seymour Hersh, anaamini kwamba Poland, Romania na nchi nyingine za ukanda huo zinazama katika silaha ambazo zilipaswa kuingizwa Ukraine. Wakati huo huo, inasemekana kuwa silaha za Magharibi zinauzwa na makamanda wa Ukraine kwa njia ya magendo nchini Poland, Romania na nchi zingine.

Seymour Hersh

Nukta nyingine ya kupewa mazingatio ni kwamba, nchi za Magharibi zina habari kamili kuhusu biashara ya magendo ya silaha nchini Ukraine, kwa sababu ripoti kadhaa kuhusu shehena za silaha zilizotoweka zimechapishwa katika vyombo vya habari vya Marekani. Hata hivyo, vyombo vya habari kimsingi vinaunga mkono msimamo wa serikali ya Marekani na vinajaribu kuficha ukweli wa vita vya Ukraine na uhalifu wa Marekani nchini Ukraine, ambao athari zake mbaya zinaiathiri Afrika.

Maafisa wa serikali ya Russia pia wamekuwa wakionya mara kwa mara kuhusu utoroshaji wa silaha za Magharibi nje ya mipaka ya Ukraine; Suala ambalo wanasema limevuruga zaidi usalama katika maeneo mengine ya dunia.