-
Silaha za Magharibi huko Ukraine zinavuruga usalama barani Afrika
Sep 01, 2024 03:35Mwakilishi wa Kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa, Issa Konfourou, ametangaza kwamba silaha nyingi za nchi za Magharibi ambazo hutolewa kwa Ukraine zinapelekwa katika eneo la Sahel barani Afrika na kuchochea uhalifu na ugaidi.
-
Waziri Mkuu wa Senegal ataka kutengwa, kususiwa Israel
Sep 01, 2024 03:14Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko ameziasa nchi za Kiislamu kuususia utawala wa Israel na kuzidisha mashinikizo ya kulitenga dola hilo la Kizayuni.
-
Mafuriko yaua makumi ya watu nchini Niger
Sep 01, 2024 03:14Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 20 na kujeruhi makumi ya wengine katika eneo la Maradi, kusini mwa Niger.
-
Wafuasi wa chama cha Jacob Zuma wapoteza maisha katika ajali
Aug 31, 2024 23:25Wafuasi sita wa chama cha upinzani cha MK kinachoongozwa na Jacob Zuma nchini Afrika Kusini, wamepoteza maisha kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea siku ya Jumamosi, mashariki mwa nchi hiyo.
-
Ethiopia yataka juhudi za pamoja za kudumisha amani katika Pembe ya Afrika
Aug 31, 2024 22:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia ametoa mwito wa kuwepo juhudi za pamoja kati ya nchi za Pembe ya Afrika katika kupambana na al-Shabaab nchini Somalia.
-
WHO: Chanjo za mpox kuwasili hivi karibuni DRC
Aug 31, 2024 22:52Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa shehena ya kwanza ya chanjo ya virusi vya homa ya nyani (mpox) inatarajiwa kuwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika siku chache zijazo.
-
Baada ya wanajeshi 200, sasa Rais wa Rwanda awastaafisha kwa nguvu zaidi ya wanajeshi 1,000 wengine
Aug 31, 2024 09:33Rais Paul Kagame wa Rwanda ameidhinisha kustaafu zaidi ya wanajeshi 1,000 kutoka jeshini, wakiwemo majenerali watano, ikiwa ni siku moja baada ya kuwafuta kazi wanajeshi wengine zaidi ya 200 wakiwemo wa ngazi za juu.
-
Ujerumani yaondoa wanajeshi wake wa mwisho Niger baada ya kutimuliwa
Aug 31, 2024 07:29Ujerumani imeviondoa vikosi vyake vya kijeshi kutoka nchi ya Niger katika eneo lenye machafuko la Sahel barani Afrika.
-
Kesi za Mpox Nigeria zafika 48, zimeenea katika mji mkuu, majimbo 20
Aug 31, 2024 04:38Kesi za ugonjwa wa Mpox nchini Nigeria zimeongezeka hadi 48, huku virusi hivyo sasa vikiripotiwa katika mji mkuu Abuja na majimbo mengine 20.
-
Wahamiaji waliotelekezwa waokolewa karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria
Aug 31, 2024 04:37Kundi la haki za binadamu nchini Tunisia limesema limewapatia hifadhi wahajiri na wahamiaji 28 mbao waliachwa bila maji na chakula karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria.