-
Ujerumani yaondoa wanajeshi wake wa mwisho Niger baada ya kutimuliwa
Aug 31, 2024 07:29Ujerumani imeviondoa vikosi vyake vya kijeshi kutoka nchi ya Niger katika eneo lenye machafuko la Sahel barani Afrika.
-
Kesi za Mpox Nigeria zafika 48, zimeenea katika mji mkuu, majimbo 20
Aug 31, 2024 04:38Kesi za ugonjwa wa Mpox nchini Nigeria zimeongezeka hadi 48, huku virusi hivyo sasa vikiripotiwa katika mji mkuu Abuja na majimbo mengine 20.
-
Wahamiaji waliotelekezwa waokolewa karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria
Aug 31, 2024 04:37Kundi la haki za binadamu nchini Tunisia limesema limewapatia hifadhi wahajiri na wahamiaji 28 mbao waliachwa bila maji na chakula karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria.
-
Rais wa Rwanda awafuta kazi wanajeshi zaidi ya 200 wakiwemo maafisa wa ngazi za juu
Aug 31, 2024 00:45Rais Paul Kagame wa Rwanda amewafuta kazi wanajeshi zaidi ya 200 wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), wakiwemo maafisa 21 waandamizi na wa vyeo vya chini.
-
Niger na Nigeria zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama licha ya mivutano iliyopo baina yao
Aug 30, 2024 05:53Niger na Nigeria zimesaini mkataba mpya wa ushirikiano wa kiusalama licha ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili jirani kuingia doa kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea mwaka jana nchini Niger.
-
Mahakama ya ICC kuanza kusikiliza kesi ya Joseph Kony Oktoba 15
Aug 30, 2024 03:51Kesi dhidi ya mbabe wa kivita Joseph Kony anayekabiliwa na tuhuma za jinai dhidi ya binadamu itaanza kusikilizwa katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu.
-
Nigeria: BRICS inayahamasisha mataifa ya Afrika
Aug 29, 2024 23:09Balozi wa Manispaa ya Kimataifa ya BRICS (IMBRICS) nchini Nigeria amesema jumuiya ya kiuchumi ya BRICS imekuwa chanzo kikubwa cha motisha na hamasa kwa nchi nyingi za Afrika, kwa kuwa inazihimiza kupigania uhuru wao na kupinga ushawishi na ubeberu wa Magharibi.
-
Ethiopia yaingiwa na kiwewe baada ya jeshi la Misri kuingia Somalia
Aug 29, 2024 08:25Ethiopia siku ya Jumatano ilijibu kwa hasira taarifa za kuingia jeshi la Misri nchini Somalia, hatua ambayo inaashiria kuenea mvutano baina ya nchi hizo mbili jirani katika Pembe ya Afrika.
-
Burundi yaomba msaada huku watu 193 wakilazwa hospitalini kwa maradhi ya Mpox
Aug 29, 2024 08:22Wizara ya Afya ya Umma ya Burundi imesema watu 193 wamelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa Mpox huku ikihamasisha umma kukomesha kuenea kwa ugonjwa huo.
-
Afrika kupata chanjo za mpox karibu milioni moja
Aug 29, 2024 04:12Wakala wa Afya wa Umoja wa Afrika jana ulieleza kuwa unakaribia kupata karibu dozi milioni moja za chanjo ya mpox, na kuwataka wazalishaji kuzipatia taasisi nyingine teknolojia ya kutengeneza chanjo ya mpox ili kukabiliana na ugonjwa huo.