Aug 30, 2024 02:39 UTC
  • Nigeria: BRICS inayahamasisha mataifa ya Afrika

Balozi wa Manispaa ya Kimataifa ya BRICS (IMBRICS) nchini Nigeria amesema jumuiya ya kiuchumi ya BRICS imekuwa chanzo kikubwa cha motisha na hamasa kwa nchi nyingi za Afrika, kwa kuwa inazihimiza kupigania uhuru wao na kupinga ushawishi na ubeberu wa Magharibi.

Hayo yamesemwa na Samsondeen Olagunju anayewakilisha BRICS ya Manispaa ya Kimataifa (IMBRICS) katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ambayo ina jukumu la kuimarisha ushirikiano kati ya wanasiasa, wanasayansi, watendaji wakuu wa mashirika, na washikadai wengine kwa nia ya kufikia malengo ya kimkakati ya pamoja.

Amesema hayo katika mahojiano na Russia Today na kuongeza kuwa: Ushirikiano huu umekuwa chanzo cha hamasisho kwa nchi nyingi hasa za Afrika. BRICS imedhihirisha kwa mataifa ya bara hilo kwamba yanaweza kustawi, hata katika kukabiliana na vikwazo vya Magharibi. Tulihitaji tu mtu wa kutuonyesha mwanga. BRICS hadi sasa imeonyesha mwanga barani Afrika.

Mwakuilishi huyo wa BRICS nchini Nigeria amezitaja nchi kama Burkina Faso, Mali, na Niger kama mifano ya mataifa ya Afrika yanayosimama kutetea haki zao. "Wanasimamia na kupigania kile ambacho ni chao," ameeleza Olagunju.

Bendera za nchi wanachamwa wa BRICS

Jumuiya ya Kiuchumi ya BRICS inaundwa na Brazil, Russia, India, China, Afrika Kusini, Iran, Misri, Ethiopia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Nchi nyingi zikiwemo za Afrika zimetuma maombi ya kujiunga na jumuiya hiyo.

Hivi karibuni pia, Agegnehu Teshager, Spika wa Bunge la Ethiopia alisema aghalabu ya nchi za Afrika zina hamu ya kuwa wanachama wa kundi la BRICS la mataifa yanayoinukia kiuchumi duniani. Kadhalika alikosoa muundo wa sasa wa nidhamu ya dunia, na kuutaja kuwa usio wa kiadilifu. Amesema, "Dunia hivi sasa haina uadilifu, kama unavyofahamu, kuanzia muundo wa Umoja wa Mataifa hadi Baraza la Usalama la umoja huo.

Tags