-
Maporomoko ya ardhi yanatishia watu 400,000 kaskazini mwa Ethiopia
Aug 29, 2024 03:50Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo la kaskazini la Amhara nchini Ethiopia zimewaweka watu 400,000 katika hatari ya mafuriko na maporomoko ya ardhi.
-
Namibia: Hatutoruhusu meli ya silaha za Israel kutia nanga nchini kwetu
Aug 28, 2024 23:24Meli ya MV Kathrin iliyokuwa ikisafiri kutoka Vietnam imenyimwa kibali cha kutia nanga katika Bandari ya Walvis, pwani ya Namibia, huku Waziri wa Sheria wa Namibia akisema kuwa nchi yake inafungamana na wajibu wa kutounga mkono au kuhusika katika uhalifu wa kivita wa Israel.
-
Msumbiji yawaachia huru mabaharia kumi wa Kiirani
Aug 28, 2024 23:21Mabaharia 10 wa Iran waliokuwa wanashikiliwa nchini Msumbiji wameachiliwa huru.
-
Baraza la Usalama kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wa wapiganaji wa RSF
Aug 28, 2024 23:20Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linafikiria kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wawili wa kundi la wapiganaji wa RSF nchini Sudan.
-
Senegal yasitisha kwa muda uchimbaji madini kwenye mpaka wake na Mali
Aug 28, 2024 11:51Serikali ya Senegal imetangaza kuwa, imesimamisha kwa muda wa miaka mitatu shughuli za uchimbaji madini kwenye ukingo wa mto ambao ni sehemu ya mpaka wake wa kusini mashariki na Mali, kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kulinda afya ya wenyeji.
-
Wiki za mafuriko nchini Nigeria, kwa uchache watu 170 wamethibitishwa kupoteza maisha
Aug 28, 2024 02:54Takriban watu 170 wamethibitishwa kupoteza maisha na karibu 2,000 wamejeruhiwa katika matukio yanayohusiana na mvua na mafuriko kwenye kona zote za Nigeria katika kipindi cha wiki mbili za mafuriko. Zaidi ya watu 205,300 wamelazimika kuhama makazi yao.
-
Raila atangaza rasmi kuwania uenyekiti wa Umoja wa Afrika
Aug 28, 2024 00:55Raila Odinga, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani jana Jumanne alitangaza rasmi kugombea uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
-
Umoja wa Mataifa walalamikia maamuzi ya upande mmoja yanayohatarisha amani nchini Libya
Aug 28, 2024 00:49Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) umelalamikia uamuzi wa upande mmoja wa Benki Kuu ya Libya hasa wakati huu ambapo hali inazidi kuwa mbaya nchini humo kutokana na maamuzi ya upande mmoja ya mirengo kisiasa.
-
WHO yazindua mpango wa miezi sita wa kuzuia usambaaji wa Mpox
Aug 27, 2024 03:27Shirika la Afya Duniani WHO limezindua mpango wa miezi sita wa kusaidia kukomesha usambaaji wa maambukizi ya ugonjwa wa mpox.
-
Wananchi wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya rais iliyogharimu dola milioni 100
Aug 26, 2024 22:41Ununuzi wa hivi karibuni wa ndege mpya ya Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, iliyogharimu dola za Kimarekani milioni 100 umewakasirisha sana wananchi wa nchi hiyo.