Mahakama ya ICC kuanza kusikiliza kesi ya Joseph Kony Oktoba 15
Kesi dhidi ya mbabe wa kivita Joseph Kony anayekabiliwa na tuhuma za jinai dhidi ya binadamu itaanza kusikilizwa katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Inaeelezwa kuwa, vikao vya kusikiliza kesi hiyo vimepangwa kuanzia Oktoba 15 kuandaa kesi ya mashtaka yanayomkabili Joseph Kony wakati bado anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Hata hivyo katika ombi lililowasilishwa Alkhamisi ya jana Agosti 29, 2024, mawakili wake walioteuliwa na mahakama wanapinga.
Upande wa utetezi wa kiongozi wa Lord's Resistance Army (LRA), anayeshitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa kati ya mwaka 2002 na 2005 kaskazini mwa Uganda, unawatuhumu majaji kwa kupuuza swali kuu: Je Joseph Kony angali hai?
Mawakili hao wanahakikisha kuwa kesi hiyo haiko tayari. Mwendesha mashtaka anapaswa kuwakabidhi mawakili kurasa zote takriban 100,000 za faili ambazo zinahusiana na makosa 36 ya mashtaka yaliyotekelezwa na uoga uliosababishwa na wanamgambo waliotekeleza uhalifu wao kwa kukata midomo na masikio ya waathiriwa.
Wakiongozwa na mbabe wa kivita aliyeko mafichoni Joseph Kony, waasi wa LRA waliwatia hofu Waganda kwa takriban miaka 20 wakipigana na serikali ya Rais Yoweri Museveni kutoka kambi za kaskazini mwa Uganda na nchi jirani. Wanamgambo hao wameangamizwa kwa kiasi kikubwa, lakini Kony anasalia kuwa mmoja wa watoro wanaosakwa sana na mahakama ya ICC.
Genge la Kikristo na la kigaidi la LRA lilianzishwa na Mkatoliki Joseph Kony miongo mitatu iliyopita ambapo Kony alijiita pia nabii.