Aug 31, 2024 08:07 UTC
  • Wahamiaji waliotelekezwa waokolewa karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria

Kundi la haki za binadamu nchini Tunisia limesema limewapatia hifadhi wahajiri na wahamiaji 28 mbao waliachwa bila maji na chakula karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria.

Kundi la kutetea haki za binadamu la nchini Tunisia kwa jina la Tunisian Forum for Economic and Social Rights Group (FTDES) limesema katika taarifa yake kuwa "timu yao imewakuta watu 28 katika hali mbaya ya kibinadamu, bila maji wala chakula chochote," 

Wanawake saba, watatu kati yao wakiwa wajawazito, na watoto wawili ni miongoni mwa wale waliopatiwa msaada na kundi la kutetea haki za binadamu la Tunisia miongoni mwa watu 42 walioripotiwa kuhama makazi yao na kutelekezwa katika eneo la mpakani  jangwani. 

Romdhane Ben Amor msemaji wa kundi la kutetea haki za binadamu la nchini Tunisia amesema kuwa wahajiri wengine kadhaa "wamejificha kwa kuhofia polisi.

Juzi Alhamisi makundi ya kutetea haki za binadamu yalisema kuwa wahajiri na raia wanaotafuta hifadhi walifukuzwa katika mji wa pwani wa Sfax huko Tunisia, ambao ni kituo kikuu ambako wahajiri huanza safari zao kuelekea Italia, na kisha maafisa husika wa Tunisia wahawahamisha hadi katika jimbo la Gafsa, linalopakana na Algeria kusini magharibi mwa Tunisia na kuwaacha hapo. 

Tunisia ni kituo muhimu cha kuondokea wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterania kuelekea barani Ulaya kwa ajili ya kutafuta maisha bora. 

 

Tags