China yaitahadharisha Marekani kuhusu vita dhidi ya Iran
-
Fu Cong
China imetahadharisha kwamba hatua hatari za kijeshi zinazoongozwa na Marekani dhidi ya Iran zinaweza kuyumbisha eneo la magharibi mwa Asia na kuisukuma kanda hiyo kwenye matokeo yasiyotabirika.
Akizungumza jana katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Fu Cong, Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa alisema hali ya mambo inayoizunguka Iran sasa imeibua wasiwasi duniani kwa kuzingatia vitisho vya vita vinavyoongozeka na mivutano ya kikanda inayoshtadi.
Fu Cong ametahadharisha kuwa hatua hatari za kijeshi zitakuwa na matokeo haribifu na kusisitiza kwamba matumizi ya nguvu hayawezi kutatua matatizo. "Hatua yoyote hatari ya kijeshi italisogeza eneo hilo katika shimo la maafa," amesema Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa.
Fu pia ameitaka Washington na washirika wake kuacha kuchochea mgogoro na kusisitiza kuwa China inatumai kwamba Marekani na pande nyingine husika zitatii wito wa jamii ya kimataifa na nchi za kanda ya Magharibi mwa Asia na kuchukua hatua muhimu kwa amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati, na kucha kuzidisha mivutano na kuchochea moto wa mgogoro.
Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa ametilia mkazo haki ya Iran ya kujitawala na kusisitiza kuwa mustakbali wa Iran unapasa kuamuliwa na Wairani wenyewe.
Balozi Fu Cong pia amesema Beijing inaunga mkono utulivu, umoja wa kujitawala, usalama na umoja wa ardhi nzima ya Iran.
Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa ameeleza haya kufuatia matamshi ya vitisho ya Donald Trump ambaye hivi karibuni alitishia kufanyya hujua mpya ya kijeshi ya Iran.
Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi, Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wiki iliyopita alisisitiza kuwa Iran imejianda kikamilifu kutoa jibu kali kwa chokochoko zozote dhidi ya nchi hii na kuwaonya maadui dhidi ya hatua zao za kijuba.