-
Baraza la Usalama la UN lawaadhibu makamanda wa RSF kwa ukatili wa Darfur
Feb 26, 2026 23:19Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea vikwazo makamanda wanne wa kundi la waasi la Rapid Support Forces (RSF) linalopigana na jeshi la Sudan, wanaoshukiwa kufanya ukatili dhidi ya raia ambao wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema ulikuwa na "ishara za mauaji ya kimbari."
-
Senegal inapendekeza sheria kali zaidi dhidi ya vitendo vya mahusiano ya jinsia moja
Feb 26, 2026 07:26Waziri Mkuu wa Senegal amependekeza sheria mpya itakayoongeza adhabu dhidi ya mahusiano ya jinsia moja, ambapo watakaopatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka kumi jela.
-
Makumi wauawa katika mashambulizi pacha ya magaidi Nigeria
Feb 26, 2026 01:40Watu wasiopungua 25 wameuawa huku nyumba kadhaa zikichomwa moto baada ya watu wenye silaha kushambulia vijiji viwili katika Jimbo la Adamawa, kaskazini mashariki mwa Nigeria usiku wa kuamkia jana.
-
Waafrika 1,700 wadaiwa kushiriki katika vita vya Russia, Ukraine
Feb 26, 2026 01:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha amedai kwamba, zaidi ya Waafrika 1,700 wanapigana kwa niaba ya Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, na kuongeza kwamba Moscow inatumia hadaa kuwasajili jeshini raia hao wa Kiafrika.
-
Tanzania yatoa tahadhari ya kuongezeka maambukizi ya mafua, Covid 19 na Dengue
Feb 26, 2026 00:14Wizara ya Afya ya Tanzania imetoa tahadhari ya afya kwa umma ya kuongezeka kwa maambukizi ya mafua na Uviko-19 na kuongezeka kwa hatari ya homa ya dengue, huku ikiwataka wananchi kuchukua hatua za haraka za kujikinga hasa katika kipindi cha msimu wa mvua.
-
Kampuni ya Mali yachukua vituo vya mafuta vya TotalEnergies
Feb 25, 2026 23:51Kampuni ya NDC Energie ya Mali imenunua takriban vituo 80 vya mafuta nchini Mali ambavyo awali vilikuwa vinaendeshwa na shirika la Ufaransa la TotalEnergies.
-
UN yalaani mashambulizi ya RSF huko Sudan, yataka vita vikomeshwe
Feb 25, 2026 05:53Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) limeelezea "wasiwasi mkubwa" kuhusu kuongezeka kwa ghasia na machafuko katika nchi iliyoathiriwa ba vita ya Sudan, hasa katika majimbo ya Darfur na Kordofan, likitaka mapigano yasitishwe mara moja.
-
Al-Burhan atoa fursa ya msamaha kwa wapiganaji wa RSF watakaoweka silaha zao chini
Feb 25, 2026 03:29Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ametangaza fursa ya msamaha kwa wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) ikiwa wataweka silaha zao chini.
-
UN yatoa wito wa msaada wa dharura kwa wakimbizi wa Burundi waliopo na wanaorudi nchini
Feb 25, 2026 03:28Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, (UNHCR) limetangaza kuwa, ufadhili endelevu na wa uhakika unahitajka ili kuendeleza ulinzi kwa wakimbizi na kusaidia urejeaji na ujumuishaji wa raia wanaorudi nchini Burundi, wakati huu ambapo kambi zinzowahifadhi zinakabiliwa na msongamano mkubwa na uhaba wa huduma muhimu.
-
Takriban watu milioni 6.5 wanakabiliwa na njaa kali kutokana na ukame ulioikumba Somalia
Feb 25, 2026 00:57Serikali ya Somalia na Umoja wa Mataifa zimetangaza kuwa wananchi wa Somalia wasiopungua milioni 6.5 wanakabiliwa na njaa kali kutokana na ukame ulioiathiri nchi hiyo.