-
Rais Samia: Ghasia za uchaguzi zinaweza kuathiri upatikanaji wa fedha
Nov 19, 2025 03:28Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania jana alisema kuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 zinaweza kuathiri upatikanaji wa ufadhili wa kimataifa kwa nchi hiyo.
-
Onyo la Afrika Kusini kuhusu njama ya kuwahamisha Wapalestina kwa nguvu
Nov 18, 2025 22:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema kuwasili Johannesburg wiki iliyopita kwa ndege iliyobeba wakimbizi wa Kipalestina ni “operesheni iliyopangwa waziwazi” ya kuwahamisha Wapalestina.
-
Mkuu wa jeshi la Nigeria aagiza kutafutwa usiku na mchana mabinti wa shule waliotekwa nyara
Nov 18, 2025 22:53Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria ameviagiza vikosi vya jeshi hilo kuendesha msako wa "usiku na mchana" ili kuwanusuru mabinti 25 wa shule waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
-
Kwa nini Afrika Kusini imedhamiria kufuatilia kesi ya mauaji ya halaiki huko Gaza?
Nov 18, 2025 22:42Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa tuhuma za kutenda mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Wagonjwa ni kati ya watu karibu 30 waliouawa katika shambulio la waasi mashariki mwa Kongo
Nov 18, 2025 07:28Takriban watu 29, wakiwemo wagonjwa wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) ambalo lililenga kituo cha afya na vijiji kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Jeshi la Sudan laondoka "Umm Sayala" huku mapigano makali yakiendelea Kordofan
Nov 18, 2025 03:36Chanzo cha kijeshi kimethibitisha kwamba jeshi la Sudan na vikosi washirika jana Jumatatu viliondoka katika mji wa Umm Sayala huko Darfur Kaskazini, saa chache baada ya kuukomboa kutoka kwa wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), huku mapigano yakiiendelea katika maeneo kadhaa ya eneo hilo.
-
Nchi za Maziwa Makuu zaitangaza RSF kuwa ni kundi la kigaidi
Nov 17, 2025 22:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imetangaza kwamba Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu uliofanyika Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeidhinisha pendekezo la kuvitangaza Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF kuwa ni "kundi la kigaidi."
-
Kiongozi wa Kijeshi wa Madagascar alihutubia taifa kwa mara ya kwanza
Nov 17, 2025 22:51Karibu mwezi mmoja baada ya kuapishwa kuwa "rais wa mpito" wa Madagascar, Michael Randrianirina kwa mara ya kwanza amelihutubia taifa akiwa na shauku na hamasa kubwa na kutoa ahadi nyingi kwa wananchi.
-
Kiwanda cha kwanza cha kampuni ya Israel ya uundaji droni za Spike chafunguliwa nchini Morocco
Nov 17, 2025 07:18Kampuni moja ya utawala wa kizayuni wa Israel imefungua kiwanda chake cha kwanza nje ya nchi huko Morocco cha uundaji wa ndege zisizo na rubani za mashambulizi aina ya Spike.
-
Afrika Kusini yaanza kufufua miradi ya nyuklia
Nov 17, 2025 05:44Afrika Kusini imeamua kufufua miradi ya nyuklia iliyokwama kwa muda mrefu na kufungua tena vituo muhimu vya utafiti, kama sehemu ya juhudi za kujenga upya utaalamu wa ndani na kujipanga upya katika masoko yanayochipuka ya mafuta ya mitambo ya nyuklia duniani.