-
Afrika Kusini imejiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 uliosusiwa na Marekani
Nov 19, 2025 23:49Afrika Kusini inajiadaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20, unaowakutanisha viongozi kutoka mataifa tajiri duniani, kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumu na kisiasa. Maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika sikuu za Jumamosi na Jumapili ijayo yamekamilika.
-
Wapalestina wa Gaza waelezea safari yao ya siri kuelekea Afrika Kusini katika njama iliyotekelezwa na Israel
Nov 19, 2025 23:27Wapalestina walioondoka Gaza hivi karibuni kupitia njia fiche ya uhamishaji inayodaiwa kuunganishwa na ofisi ya wizara ya vita ya Israel wanasema walipelekwa nje ya eneo hilo linalokumbwa na vita bila taarifa, hati, au hata kuelewa walikokuwa wanaelekezwa.
-
Maafisa wawili wa Kenya wauawa katika hujuma ya magaidi wa al-Shabaab karibu na mpaka wa Somalia
Nov 19, 2025 23:27Maafisa wawili wa Kitengo cha Ulinzi wa Mpaka cha Kenya wameuawa Jumatano baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini (IED) lililowekwa na magaidi wakufurishaji wa al-Shabaab kutoka Somalia katika barabara ya Liboi kuelekea Kulan, kaskazini mwa Kenya.
-
Eswatini ilipokea hongo ya dola milioni 5 kutoka Marekani ili kukubali wahamiaji waliotimuliwa
Nov 19, 2025 23:26Eswatini imethibitisha kupokea dola milioni 5.1 kutoka Washington kama sehemu ya makubaliano ya kupokea wahamiaji waliofukuzwa Marekani licha ya kutokuwa na uhusiano wowote na taifa hilo la kusini mwa Afrika.
-
Katibu Mkuu wa UN: Ugaidi katika eneo la Sahel ni tishio linaloongezeka
Nov 19, 2025 09:05Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewatahadharisha viongozi duniani kwamba ugaidi katika eneo la Sahel barani Afrika ni tishio linaloongezeka duniani.
-
Rais wa Nigeria athibitisha kuuawa afisa wa ngazi ya juu wa jeshi
Nov 19, 2025 08:54Rais wa Nigeria amethibitisha kuwa Brigedia jenerali Musa Uba ameuawa na kundi la kigaidi akiwa matekani. Mauaji hayo yamefanywa siku chache baada ya afisa huyo wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la ISWAP kufuatia shambulio la kuvizia kaskazini mashariki mwa Jimbo la Borno ambalo pia liliwaua wanajeshi wanne.
-
Rais Samia: Ghasia za uchaguzi zinaweza kuathiri upatikanaji wa fedha
Nov 19, 2025 03:28Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania jana alisema kuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 zinaweza kuathiri upatikanaji wa ufadhili wa kimataifa kwa nchi hiyo.
-
Onyo la Afrika Kusini kuhusu njama ya kuwahamisha Wapalestina kwa nguvu
Nov 18, 2025 22:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema kuwasili Johannesburg wiki iliyopita kwa ndege iliyobeba wakimbizi wa Kipalestina ni “operesheni iliyopangwa waziwazi” ya kuwahamisha Wapalestina.
-
Mkuu wa jeshi la Nigeria aagiza kutafutwa usiku na mchana mabinti wa shule waliotekwa nyara
Nov 18, 2025 22:53Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria ameviagiza vikosi vya jeshi hilo kuendesha msako wa "usiku na mchana" ili kuwanusuru mabinti 25 wa shule waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
-
Kwa nini Afrika Kusini imedhamiria kufuatilia kesi ya mauaji ya halaiki huko Gaza?
Nov 18, 2025 22:42Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa tuhuma za kutenda mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.