-
Wanachuo wa Tehran wakusanyika kulalamikia kuendelea kushikiliwa korokoroni Sheikh Ibrahim Zakzaky
Jul 15, 2019 06:54Wanachuo wa vyuo vikuu hapa mjini Tehran leo wamefanya mkusanyiko mkubwa kulalamikia kuendelea kushikiliwa korokoroni Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
-
Rais Rouhani: Njama zote za Marekani dhidi ya Iran zimegonga mwamba
Jul 14, 2019 22:37Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika kipindi cha miezi 14 iliyopita, Marekani imetekeleza vikwazo vikali kabisa dhidi ya taifa la Iran, hata hivyo imeshindwa katika nyanja zote iwe ni katika uga wa kijamii, kisiasa na kadhalika.
-
Zarif: Iran ina nia ya kweli ya kuyalinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA
Jul 14, 2019 22:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mara baada ya kuwasili New York, Marekani kwamba Tehran ina nia ya kweli ya kushirikiana na nchi za Ulaya katika kuyalinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran: Hakuna mazungumzo yoyote baina yetu na Marekani
Jul 14, 2019 06:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran haifanyi mazungumzo ya kiwango chochote kile na viongozi wa Marekani.
-
Rouhani: Bodi ya IAEA imepuuza njama za Marekani dhidi ya Iran
Jul 14, 2019 03:05Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya kuendelea kutengwa Marekani katika uga wa kimataifa na kusema kuwa, mbali na nchi moja au mbili, nchi zote wanachama wa Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) katika kikao chao cha hivi karibuni zilipuuza njama za Marekani dhidi ya Iran.
-
Zarif: Liwe liwalo, Iran itaendelea kuuza mafuta yake nje
Jul 14, 2019 02:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo haramu vya Marekani dhidi ya taifa hili na kusisitiza kuwa, Tehran itaendelea kuyauza mafuta yake nje ya nchi bila kubabaishwa na chochote.
-
El Baradei akosoa siasa za Donald Trump dhidi ya Iran
Jul 13, 2019 06:41Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amekosoa vikali hatua ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile sera za nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Tehran yaitaka Uingereza ijiepushe na mchezo hatari, iiachilie meli ya mafuta ya Iran
Jul 12, 2019 20:37Iran imeitaka Uingereza iachilie mara moja meli yake kubwa ya mafuta iliyokamatwa katika lango bahari la Jabal Tariq (Gibraltar) na imeitahadharisha London juu ya kuingia katika mchezo hatari usio na mwisho.
-
Iran: Israel isitutishe na F-35, jibu letu kwa chokochoko zake litakuwa kali
Jul 12, 2019 11:10Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya vitisho ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, jibu la taifa hili dhidi ya chokochoko za maadui litakuwa kali na la kuumiza.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran: Ulaya inafuata Marekani katika kadhia ya JCPOA
Jul 12, 2019 10:51Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa nchi za Ulaya zilizotia saini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na Iran hivi sasa na mwaka mmoja baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo ya kimataifa hazijatekeleza majukumu yao katika makubaliano hayo na kivitendo zimeifuata Marekani.