El Baradei akosoa siasa za Donald Trump dhidi ya Iran
(last modified Sat, 13 Jul 2019 11:11:26 GMT )
Jul 13, 2019 11:11 UTC
  • Muhammad el Baradei
    Muhammad el Baradei

Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amekosoa vikali hatua ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile sera za nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Muhammad el Baradei amekosoa vikali hatua ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano hayo ya kimataifa katika mazungumzo yake na shirika la utangazaji la BBC la Uingereza na kusema: "Washington inatumia mbinu ya kutaka kuigharikisha Iran."

El Baradei amesema: "Wamarekani wanatumia mbinu bandia ya kuigharikisha Iran kisha wanaiangalia nchi hiyo na kuiambia njooni tufanye mazungumzo bila ya masharti yoyote."  

Muhammad el Baradei

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa wakala wa IAEA amekadhibisha madai yanayosema kwamba, Iran inakaribia kuwa tishia la silaha za nyuklia na kusema: Hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya kurutubisha madini ya urani kwa daraja 4.5 zaidi ya daraja 3.67 iliyoainishwa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA bado iko mbali sana hadi kufikia kiwango cha daraja 90 zinazohitajika kuweza kutengeneza bomu la nyuklia. 

Iran imechukua uamuzi wa kurutubisha madini ya urani kwa daraja 4.5 zaidi ya daraja 3.67 baada ya kumalizika muhula wa siku 60 uliokuwa umetolewa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa kwa nchi zilizotia saini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa vipengee vya makubaliano hayo.   

Tags