-
Iran yamuita balozi wa Nigeria nchini kuhusu hali ya Sheikh Zakzaky
Jul 09, 2019 03:53Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imemuita balozi mdogo wa Nigeria hapa mjini Tehran na kumkabidhi malalamiko rasmi pamoja na kumueleza wasiwasi wa taifa hili kuhusu ripoti zinazoashiria kuwa mbaya zaidi hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
-
Hatua ya pili; kiwango cha urutubishaji urani ni cha kudhamini mahitaji ya Iran na sio ya JCPOA
Jul 08, 2019 07:14Baada ya kumalizika muhula wa kwanza wa siku 60 zilizotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa anchi za Ulaya ili zitekeleze ahadi zao za mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA, Tehran imetangaza kuanza hatua ya pili ya kupunguza ahadi zake kwa mujibu wa vipengee vya 26 na 36 vya mapatano hayo, kwa kuongeza kiwango cha urutubishaji wake wa madini ya urani.
-
Iran: Tutachukua hatua kubwa zaidi kama nchi za Ulaya zitaendelea kukwepa majukumu yao + Video
Jul 08, 2019 07:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kama nchi zilizobakia katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hasa za Ulaya zitaendelea kukwepa kutekeleza majukumu yao, basi Tehran itaingia kwa nguvu kubwa zaidi katika awamu ya tatu ya kupunguza utekelezaji wa ahadi zake ndani ya mapatano hayo.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Hatutaruhusu uharamia wa Uingereza
Jul 08, 2019 02:15Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya askari wa Jeshi la Wanamaji la Uingereza ya kuisimamisha meli ya mafuta ya Iran katika Lango Bahari la Jabal al Tariq (Gibraltar) na kueleza bayana kuwa, Tehran kamwe haitaruhusu uharamia huo wa London.
-
Iran: Ni haki yetu kuchukua hatua za kukabiliana na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani
Jul 07, 2019 22:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ni haki ya Tehran kuchukua hatua za kisheria ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA katika kukabiliana na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi yake.
-
Iran yaingia hatua ya pili ya kupunguza uwajibikaji wake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Jul 07, 2019 07:43Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo imetangaza kuanza kutekeleza hatua ya pili ya kupunguza uwajibikaji wake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Rouhani amwambia Macron: Umoja wa Ulaya utekeleze majukumu yake
Jul 06, 2019 22:31Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana usiku alifanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron ambapo amezitaka nchi za Ulaya kutekeleza majukumu yao yanayohusiana na makubaliano ya kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
-
Iran na Uganda kuimarisha uhusiano wao wa kiutamaduni
Jul 06, 2019 21:50Waziri wa Jinsia na Utamaduni wa Uganda amesema nchi hiyo ya Afrika Mashariki ina hamu ya kuimarisha uhusiano wake wa kiutamaduni na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Taasisi ya Haki za Binadamu ya Iran: UN inapaswa kuandaa mazingira ya kuachiliwa huru haraka Sheikh Zakzaky
Jul 06, 2019 06:32Taasisi ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ya Solh-e Ziba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuutaka umoja huo uandae haraka mazingira ya kuchiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ili aende akatibiwe nje ya nchi.
-
Sisitizo la Russia la nafasi hasi ya vikwazo vya Marekani katika hatua za hivi karibuni za Iran
Jul 05, 2019 23:36Russia ambayo ni moja ya wanachama muhimu wa kundi la 4+1 la mapatano ya nyuklia ya JCPOA imesisitizia haja ya kuendelezwa mapatano hayo kwa hali yoyote ile.