-
Ayatullah Kermani: Marekani inaogopeshwa sana na uwezo wa kiulinzi wa Iran
Jul 05, 2019 10:46Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amejibu matamshi ya rais wa Marekani juu ya sababu iliyoifanya Washington kujiepusha kuishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, viongozi wa Marekani wanaogopa uwezo wa kijeshi na kiulinzi wa Iran.
-
Kuisimamisha meli ya mafuta ya Iran, chokochoko za Uingereza katika uwanja wa Marekani
Jul 05, 2019 08:00Askari wa Jeshi la Wanamaji la Uingereza jana Alkhamisi waliisimamisha meli ya mafuta ya Iran katika Lango Bahari la Jabal al Tariq kwa madai kwamba ilikuwa inaelekea Syria.
-
Zarif: Hatua ya Iran kupunguza ahadi ilizojifunga nazo itazuia JCPOA kuvunjika kikamilifu
Jul 05, 2019 02:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ukiukaji ahadi wa madola ya Ulaya katika kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran na kueleza bayana kwamba, hatua ya kupunguza ahadi ilizojifunga nazo Iran kwa mujibu wa mapatano hayo inachukuliwa kwa shabaha ya kuzuia JCPOA isivunjike kikamilifu.
-
Mkuu wa IRGC: Iran imefanikiwa kuzima njama za maadui
Jul 04, 2019 09:23Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa hili mara zote limefanikiwa kuzima njama na mipango ya hali ya juu ya maadui dhidi yake.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu juu ya umuhimu wa ibada ya Hija
Jul 04, 2019 08:54Akizungumza jana Jumatano asubuhi mbele ya wasimamizi na wahudumu wa ibada ya Hija Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kuwa ibada ya Hija ni mjumuiko wa kipekee na bora wa thamani zinazoenziwa na Uislamu.
-
Russia yaunga mkono mazungumzo baina ya Iran na nchi za Kiarabu
Jul 04, 2019 02:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, anaunga mkono na kushajiisha mazungumzo baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za Kiarabu.
-
Uhispania: Iran haijavunja hata mara moja mapatano ya JCPOA
Jul 03, 2019 22:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, uamuzi wa hivi karibuni wa Iran haujavunja vipengee vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kimsingi hilo ni suala la kiufundi.
-
Amir Abdolahian: Njia ya chini ya ardhi ya Msikiti wa al Aqsa ni uvunjaji wa wazi wa haki za binadamu
Jul 03, 2019 22:11Katibu Mkuu wa Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Palestina amesema kuwa, kufunguliwa njia ya chini ya ardhi inayopitia chini ya Msikiti wa al Aqsa ni uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa na maazimio ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Serikali ya Saudia ilinde usalama na heshima ya mahujaji
Jul 03, 2019 08:44Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema leo katika hadhara ya maafisa wa Hija hapa nchini kwamba serikali ya Saudi Arabia ina wajibu na majukumu mazito ya kulinda usalama wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hadhi yao bila ya kueneza anga ya kipolisi.
-
Rais Rouhani: Kama Marekani inaogopa moto basi haipaswi kuwasha muale
Jul 03, 2019 08:31Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yana manufaa kwa mataifa yote, eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima na kuongeza kuwa, Kama Marekani inaogopa moto haipaswi kuwasha muale na itekeleze maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.