Mkuu wa IRGC: Iran imefanikiwa kuzima njama za maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54553-mkuu_wa_irgc_iran_imefanikiwa_kuzima_njama_za_maadui
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa hili mara zote limefanikiwa kuzima njama na mipango ya hali ya juu ya maadui dhidi yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2019 09:23 UTC
  • Mkuu wa IRGC: Iran imefanikiwa kuzima njama za maadui

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa hili mara zote limefanikiwa kuzima njama na mipango ya hali ya juu ya maadui dhidi yake.

Meja Jenerali Hossein Salami, kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo Alkhamisi na kueleza bayana kuwa, vikosi vya kujitolewa hapa nchini (Basiji) vimeleta mlingano wa nguvu katika kupambana na maadui wa taifa hili.

Amesema vikosi vya Basij mbali na kusambaratisha njama za madola ya uistikbari, lakini pia vimetoa mchango mkubwa katika kulinda na kutetea thamani za Uislamu.

Kamanda Mkuu wa IRGC amebainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imeonyesha kuwa ina uwezo na nguvu za kuushinda ustikabari wa kimataifa katika nyuga mbalimbali na ndiposa Marekani inekerwa na kutiwa kiwewe na ushawishi wa Iran kieneo na kimataifa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akikagua gwaride la vikosi vya Basij

Meja Jenerali Hossein Salami amefafanua kuwa, njama za madola ya kibeberu za kulitishia taifa hili ili liachane na sera yake ya muqawama zimegonga mwamba, na ndiposa hivi sasa maadui hawawezi kuthubutu kuingia katika vita na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imeonyesha kuwa ina uwezo na nguvu za kuushinda ustikabari wa kimataifa katika nyuga mbalimbali.