Sayyid Ahmad Khatami: Kujenga Matumaini ndio Nguzo Kuu ya Muqawama
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran amesema kuwa: Vyombo vya habari vya kungalia na kusikiliza lazima vitambue kuwa nguzo kuu ya kambi ya Muqawama ni kujenga matumaini.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo kwenye khutba za Sala ya Ijumaa leo hapa mjini Tehran na kufafanua kwa kusema: Imam Hadi (AS) alinukuliiwa akisiema kuwa katika vita 80 vya huko nyuma, neema ya Mwenyezi Mungu na uungaji mkono wa waumini vilichukua nafasi muhimu mno. Mtume Mtukufu (SAW) alikuwa katika hali ya vita vya mfululizo kwa muda wa miaka kumi, na katika miaka hiyo yote, waumini walibaki wakiwa tayari wakati wote. Swali linajitokeza hapa ni kwamba: Mtume aliwezaje kuwafanya watu wawe tayari kwenda vitani muda wote? Hili ni jambo tunaloliihitaji pia leo hii.
Ayatullah Ahmad Khatami pia amesema: Mtume Mtukufu (SAW) aliimarisha utamaduni [wa Muqawama], akaimarisha imani za msingi, akapanda mti imara wa matumaini katika nyoyo za askari wake, akatia hofu katika nyoyo za maadui na kukabiliana kwa ufanisi mkubwa na vita vya kisaikolojia vya adui. Mambo haya matano ndiyo yaliyodhamini ushindi wa Waislamu na kuwafanya waumini kuwa tayari wakati wote kuingia katika uwanja wa vita.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran vilevile amesema: Mtume Mtukufu (SAW) aliendeleza utamaduni wa *Jihadi* kama vile ambavyo pia maombolezo kwa ajili ya Bwana wa Mashahidi (Imam Hussein, AS) yamekuwa ni utamaduni uliokita mizizi leo hii.
Amesema: Vyombo vya habari vya kuangalia na kusikiliza lazima vitambue kuwa nguzo kuu ya Muqawama ni kuleta matumaini katika nyoyo za watu.
Ayatulla Ahmad Khatami ameongeza kuwa: Hotuba ya Rais (Pezeshkiian) katika Umoja wa Mataifa ilikuwa — kwa kweli — ni yenye mantiki, ya kuvutia na yenye ujasiri. Kwa hakika hotuba hiyo iliugeuza Umoja wa Mataifa kuwa mahakama na kutangaza ujumbe halisi wa kaulimbiu za "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel." Hotuba hiyo imeendana vyema na msimamo wa wananchi wa Iran ambao hawajaondoka mitaani kwa miezi saba na hawatofanya hivyo hadi pale adui atakapopigishwa magoti. Kwa kweli Rais (Pezeshkian) amewasilisha mantiki ya Iran kwa ulimwengu kwa kutumiai jukwaa la Umoja wa Mataifa.