Pars Today
Wakati utawala wa Kizayuni wa Israel ukidai kuwa umeshambulia maeneo 20 nchini Iran, wachambuzi wa mambo wanasema kuwa shambulio hilo lililofanyika mapema leo halilingani hata kidogo na Opereshen Ahadi ya Kweli-2 (Operation 'True Promise 2) iliyotekelezwa na Iran dhidi ya utawala huo katili majuma kadhaa yaliyopita.
Wizara za mashauri ya kigeni za Saudi Arabia, Malaysia, Pakistan na Oman zimetoa taarifa tofauti zikilaani hujuma za kijeshi za utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali hatua ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni ya kushambulia baadhi ya vituo vya kijeshi hapa nchini, na kuitaja kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Duru za kuaminiki zimeliambia shirika la habari la Tasnim kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ipo tayari na imejiandaa kujibu chokochoko za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kikosi cha ulinzi wa anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimethibitisha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya mashambulio ambayo yamelenga maeneo kadhaa katika mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam, na kusema uchokozi huo umezimwa kwa mafanikio.
Duru za kiusalama za Iran zimetangaza kuwa, sauti kubwa za miripuko zilizosikika alfajiri ya leo Jumamosi hapa Tehran zimetokana na majibu ya mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran kupiga silaha zilizorushwa dhidi ya baadhi ya maeneo ya pembeni mwa Tehran.
Kaimu Askofu Mkuu wa Wakristo wa Armenia nchini Iran amesema kuwa, wako chini ya amri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika hali zote.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa, visiwa vitatu vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo ni milki ya Iran, vilikuwa hivyo tangu zamani na vitaendelea daima kuwa hivyo katika siku za usoni.
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya raia wa Iran mjini Beirut na kuyataja kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala ya Lebanon.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Utekelezaji wa yaliyoafikiwa katika mkutano wa BRICS utasambaratisha njama za Marekani na washirika wake.