Iran yajitosheleza katika kutengeneza dawa za kutibu fibrosisi ya mapafu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135482-iran_yajitosheleza_katika_kutengeneza_dawa_za_kutibu_fibrosisi_ya_mapafu
Mkurugenzi wa utafiti na maendeleo wa kampuni inayotegemea maarifa nchini Iran ametangaza uzalishaji wa dawa ya Ofenib kwa mara ya kwanza hapa nchini, ambayo hutumika kwa wagonjwa wenye magonjwa ya mapafu ya ndani, hasa fibrosis ya mapafu.
(last modified 2026-01-14T12:06:56+00:00 )
Jan 14, 2026 12:06 UTC
  • Iran yajitosheleza katika kutengeneza dawa za kutibu fibrosisi ya mapafu
    Iran yajitosheleza katika kutengeneza dawa za kutibu fibrosisi ya mapafu

Mkurugenzi wa utafiti na maendeleo wa kampuni inayotegemea maarifa nchini Iran ametangaza uzalishaji wa dawa ya Ofenib kwa mara ya kwanza hapa nchini, ambayo hutumika kwa wagonjwa wenye magonjwa ya mapafu ya ndani, hasa fibrosis ya mapafu.

Kulingana na Shirika la Habari la Iran Press, Mohammad Karim Rezaei, kutoka Kituo cha Mawasiliano na Habari cha Makamu wa Rais wa Sayansi, Teknolojia na Uchumi Unaotegemea msingi wa Maarifa, huku akizungumzia uzalishaji wa bidhaa ya dawa "Ofenib", alisema: "Kwa kutengeneza bidhaa hii ndani ya nchi, Iran haitahitaji tena kuagiza kutoka nje na wagonjwa wataweza kupata dawa hii kwa urahisi. Kwa upande wa bei, bidhaa inayozalishwa ndani ya nchi ni takriban theluthi moja ya bei ya dawa kama hiyo ya kigeni."

Akizungumzia ufanisi uliothibitishwa wa bidhaa ya "Ofenib" ikilinganishwa na bidhaa ya sampuli ya kigeni, alisema: "mfanano wa kisayansi na utendaji kazi wa dawa hii na sampuli ya awali umethibitishwa kikamilifu kwa kufanya vipimo muhimu na kupokea idhini kutoka kwa Asasi ya a Chakula na Dawa."

Kulingana na mwanaharakati huyu wa teknolojia, kutokana na kwamba idadi ya wagonjwa wenye magonjwa ya mapafu ya ndani nchini ni kubwa ikilinganishwa na magonjwa adimu, uzalishaji wa dawa hii ndani ya nchi ni muhimu sana.

Rezaei alibainisha: "Kwa kufanikiwa kutengeneza bidhaa ya Ofenib", sio tu kwamba tatizo la upatikanaji wad awa hii kwa wagonjwa limetatuliwa, lakini pia kikwazo kikubwa katika matibabu ya kundi hili la wagonjwa kimeondolewa kwa upande wa bei na uchumi."

Ugonjwa wa Fibrosisi ya mapafu hutokea wakati tishu za mapafu zinapokuwa nene na kukakamaa kwa sababu ya makovu, hivyo kufanya iwe vigumu kwa mapafu kufanya kazi vizuri.