-
Wanafunzi wa Iran washinda medali tano katika Mashindano ya Kimataifa ya Fizikia 2025
Jul 25, 2025 23:01Timu ya wanafunzi wa shule za upili kutoka Iran imejinyakulia medali tano za fedha katika Mashindano ya 55 ya Kimataifa ya Fizikia (International Physics Olympiad - IPhO 2025) yaliyofanyika jijini Paris, Ufaransa.
-
Araghchi: Iran haitalegeza msimamo wake kuhusu mpango wa nyuklia wa amani
Jul 25, 2025 07:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesisitiza tena msimamo thabiti wa Tehran kuhusu haki yake ya kuendeleza mpango wake wa nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani, ikiwa ni pamoja na kurutubisha urani.
-
Satelaiti ya Iran, Nahid-2, yarushwa katika anga za mbali kwa mafanikio
Jul 25, 2025 07:27Satelaiti ya mawasiliano na utafiti wa anga ya Iran, Nahid-2, iliyotengenezwa kikamilifu ndani ya nchi, imerushwa kwa mafanikio kuelekea anga za mbali Ijumaa, Julai 25, kwa kutumia roketi ya Kirusi ya Soyuz.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa: Utawala wa Kizayuni umepata kipigo kikali kutoka Iran
Jul 25, 2025 07:26Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Tehran amesema kuwa utawala wa Kizayuni umepata kipigo kikali kufuatia mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran, na umebeba gharama nzito mno.
-
Iran yalaani hatua ya Wazayuni, yaonya juu ya kuangamizwa kabisa Palestina
Jul 24, 2025 23:50Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imelaani hatua ya Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset, ya kuidhinisha muswada unaoweka udhibiti wa utawala huo ghasibu katika Ukingo wa Magharibi na Bonde la Jordan.
-
Ayatullah Hamedani amwandikia Papa Leo: Tunapaswa kuwa sauti ya watu wanaodhulumiwa wa Gaza
Jul 24, 2025 08:40Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu kidini nchini Iran amemwandikia barua Papa Leo XIV akisema: "Mienendo ya kikatili na isiyo ya kibinadamu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa ni pamoja na kuzuia kupelekwa chakula na mahitaji muhimu kwa watu wa Gaza ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kidini, kibinadamu, maadili na sheria za kimataifa."
-
Helikopta ya Jeshi la Wanamaji la Iran yaitimua manowari ya US katika Bahari ya Oman
Jul 24, 2025 03:25Helikopta ya Jeshi la Wanamaji la Iran imeitimua manowari ya mashambulizi ya Marekani iitwayo USS Fitzgerald katika Bahari ya Oman, kwa kutoa ishara za onyo na hatimaye kuilazimisha ibadili mkondo wake kuelekea upande wa kusini wa eneo hilo.
-
Kwa nini Iran inachukulia juhudi za kuhuisha mfumo wa Snapback kuwa kinyume cha sheria?
Jul 23, 2025 23:09Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Kimataifa analichukulia jaribio lolote la Troika ya Ulaya la kuamilisha utaratibu wa Snapback kuwa ni jambo lisilokubalika kisheria.
-
Iran yaalani ukatili mkubwa wa sera ya njaa na mauaji ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza
Jul 23, 2025 07:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani " ukatili mkubwa" unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel, na kulaani sera ya njaa na mauaji ya utawala huo dhidi ya Wapalestina wanaotafuta misaada huko Gaza.
-
Rais: Ni 'njozi' kuutokomeza mpango wa nyuklia wa Iran; ikihitajika tutaipiga tena vikali Israel
Jul 23, 2025 03:51Rais Masoud Pezeshkian amepuuzilia mbali juhudi na uchochezi wa Marekani na washirika wake, hususan utawala wa kizayuni wa Israel, wa kushinikiza kutokomezwa mpango wa nishati ya nyuklia wa Iran.