-
Kiongozi wa Mapinduzi aipongeza timu ya miereka kwa kutwaa ubingwa wa dunia
Sep 17, 2025 10:21Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameipongeza timu ya taifa ya Iran ya mchezo wa miereka ya freestyle kwa kutwaa taji la ubingwa wa dunia katika Mashindano ya Miereka ya Dunia ya 2025 yaliyofanyika mjini Zagreb, Croatia.
-
Iran yatekeleza hukumu ya kifo dhidi ya jasusi wa Mossad ya Israel katika Vita ya Siku 12
Sep 17, 2025 08:55Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Babak Shahbazi, raia aliyekutwa na hatia ya kushirikiana na shirika la kijasusi la utawala wa Israel, Mossad, kwa kutoa taarifa nyeti kuhusu maeneo ya kiusalama ya Iran wakati wa vita ya siku 12 vya kichokozi vya utawala huo mwezi Juni.
-
Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran akutana na Bin Salman mjini Riyadh
Sep 17, 2025 03:17Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, Ali Larijani amekutana na Mwanamfalme wa Saudiam Mohammed bin Salman mjini Riyadh kujadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya kieneo.
-
Iran yalaani uingiliaji wa Marekani katika masuala yasiyoihusu
Sep 17, 2025 03:17Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa kauli kali ya kulaani unafiki, hadaa na uadui wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa kisingizio cha kumbukumbu ya machafuko ya Shahrivar mwaka 1401 Hijria Shambia na kusema kuwa huo mfano wa wazi wa uingiliaji wa masuala ya Iran ambayo hayaihusu Marekani ndewe wala sikio.
-
Bahreini: Uvamizi wa Israel dhidi ya Qatar, tishio kwa usalama wa eneo na kimataifa
Sep 16, 2025 23:13Balozi wa Iran katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi amelaani vikali uvamizi wa karibuni wa utawala wa Israel dhidi ya Qatar na kuitolea wito jamii ya kimataifa kuchukua hatua kuzuia kuendelea vitendo kama hivyo ambavyo vinatishia kila mtu katika kanda hii.
-
Rais Pezeshkian: Saudi Arabia inabeba 'jukumu zito' kwa umoja wa Waislamu dhidi ya Israel
Sep 16, 2025 08:42Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa mataifa makubwa ya Kiislamu, hasa Saudi Arabia yanabeba "jukumu zito sana" katika hali ya sasa, na kwamba kuwepo umoja kati ya nchi za Kiislamu kutazuia uchokozi wa Israel.
-
Baqaei: Rasimu ya azimio inasisitiza kuzuiwa mashambulizi dhidi ya taasisi za nyuklia za malengo ya kiraia
Sep 16, 2025 08:41Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametoa taarifa kuhusu rasimu ya azimio la Iran katika Mkutano Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unaoendelea Vienna, Austria ambayo inalenga kuzuia mashambulizi kwenye vituo vya nyuklia vinavyoendesha shughuli zake kwa malengo ya amani na ya kiraia.
-
Rais wa Iran azitahadharisha nchi za Kiislamu Doha: Hakuna nchi itakayokuwa salama na uchokozi wa Israel
Sep 16, 2025 04:12Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mashambulizi ya Israel ya Septemba 9 dhidi ya Qatar yameonyesha kuwa hakuna nchi ya Kiarabu au ya Kiislamu iliyo salama kutokana na vitendo vya uchokozi vya utawala huo.
-
Iran yatwaa taji la ubingwa wa dunia wa Miereka 2025, yaziacha nyuma Russia na Marekani
Sep 16, 2025 03:18Timu ya taifa ya mchezo wa miereka aina ya Freestyle ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Dunia ya Miereka ya mwaka 2025 yanayofanyika mjini Zagreb, Croatia kwa kunyakua jumla ya medali tano na kulitwaa taji hilo kabla ya muda wa mashindano kumalizika.
-
Eslami: Shambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran lilikuwa shambulio dhidi ya itibari ya IAEA
Sep 15, 2025 23:39Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesisitiza katika Mkutano Mkuu wa 69 wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwamba: Mashambulio ya Marekani na utawala wa Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran si tu kuwa ni jinai na uoga, bali pia ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya itibari ya Wakala huo na mfumo wake wa ulinzi.