Brigedia Jenerali Belali: Nguvu ya makombora ya Iran imeanza na mizinga
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133058-brigedia_jenerali_belali_nguvu_ya_makombora_ya_iran_imeanza_na_mizinga
Mshauri wa Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema: Kitengo cha mizinga cha Iran kiliundwa katika Operesheni Fat'h al-Mobin na baadaye Iran ikafikia kwenye utengenezaji wa makombora. Nguvu yetu ya sasa ni matunda ya miaka minane ya kujihami kutakatifu ambayo yalianzishwa na Hajj Hassan Tehrani-Moghaddam.
(last modified 2025-11-11T10:52:22+00:00 )
Nov 11, 2025 10:52 UTC
  • Brigedia Jenerali Belali: Nguvu ya makombora ya Iran imeanza na mizinga

Mshauri wa Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema: Kitengo cha mizinga cha Iran kiliundwa katika Operesheni Fat'h al-Mobin na baadaye Iran ikafikia kwenye utengenezaji wa makombora. Nguvu yetu ya sasa ni matunda ya miaka minane ya kujihami kutakatifu ambayo yalianzishwa na Hajj Hassan Tehrani-Moghaddam.

Brigedia Jenerali Ali Belali, amesema hayo katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Fars na huku akibainisha jitihada na ubunifu mkubwa wa Shahid Hassan Tehrani-Moghaddam na jukumu lake katika uundaji wa nguvu za makombora za Iran amesema kuwa: Shahid Tehrani-Moghaddam ni mmoja wa wahitimu wa chuo na maktaba ya Imam Khomeini (Mungu amrehemu), ambaye kaulimbiu yake ilikuwa ni sentensi mbili ambazo Imam alikuwa akizirudia mara kwa mara ambazo zinasema: "Mtegemee Mungu" na "Jiamini."

Ameongeza kuwa: Dua zake na kutawakali kwake kwa Maimamu watoharifu katika kuendeleza njia ya mapambano na kujiamini vilimpa mafanikio makubwa. Wakati utawala wa Saddam ulipokuwa unatushambulia kwa mabomu na makombora na wakati tulipokwenda kupata mafunzo ya kombora la Scud nchini Syria, Shahid Tahrani-Moqaddam alikuwa anasema: "Jamani, tusijifunze tu kurusha makombora ya Scud bali tujifunze namna ya kulitengeneza na kazi nyingine," na yeye mwenyewe alikuwa mstari wa mbele katika kujifunza utengenezaji wa kina wa makombora kupitia kombora hilo la Scud.

Hakuna kisichowezekana, ndiyo iliyokuwa moja ya kaulimbiu kuu za Shahid Tehrani-Moghaddam. Akizungumzia vigezo vya utu na ubinadamu vya Shahid Tehrani-Moghadam, mshauri wa Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema: Siku zote Shahid Tehrani-Moghaddam alikuwa anaangalia mbali na alikuwa imara sana katika njia ya kufikia malengo yake. Hakuna changamoto na kizuizi chochote kilichokwamisha jitihada zake.