-
Iran kurusha satelaiti tatu mpya katika anga za mbali
Sep 08, 2025 23:03Iran iko mbioni kupiga hatua kubwa katika mpango wake wa anga za mbali kwa kuzindua satelaiti tatu mpya ambazo ni Kowsar, Zafar, na Paya kabla ya mwisho wa mwaka wa Kiirani (tarehe 20 Machi, 2026).
-
Pezeshkian: Hatuna uadui na nchi yoyote ya Kiislamu na tunashikamana na umoja wa Umma wa Kiislamu
Sep 08, 2025 09:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesema Jamhuri ya Kiislamu haitazozana na taifa lolote la Kiislamu na imejizatiti kikamilifu katika kuendeleza mshikamano na umoja katika Umma wa Kiislamu.
-
Pezeshkian: Mipaka ya kijiografia kamwe haiwezi kuyatenganisha mataifa mawili ndugu ya Iran na Iraq
Sep 08, 2025 04:06Rais wa Iran ameutaja uhusiano kati ya mataifa mawili na nchi mbili za Iran na Iraq chini ya kivuli cha mifungamano ya kidini na kiutamaduni kuwa mkubwa na wa kihistoria na kusisitiza kuwa mipaka ya kijiografia kamwe haiwezi kutenganisha mataifa haya mawili ndugu.
-
Kiongozi: Mataifa ya Kiislamu lazima yavunje uhusiano na Israel kukabiliana na 'jinai za maangamizi' inazofanya Ghaza
Sep 07, 2025 23:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lazima mataifa ya dunia hususan nchi za Kiislamu zivunje uhusiano wote wa kibiashara na kisiasa na utawala wa kizayuni wa Israel ili kukabiliana na jinai zake za maangamizi unazofanya katika Ukanda wa Ghaza.
-
Araqchi: Nchi 3 za Ulaya lazima zibadili njia yao ya uharibifu
Sep 07, 2025 08:31Katika makala yake kwenye gazeti la The Guardian, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kwamba nchi tatu za Ulaya (Ufaransa, Uingereza na Ujerumani), zinapaswa kubadili mkondo wao wa uharibifu, akisisitiza kuwa: "Mchezo huu hautakuwa na matokeo yanayotarajiwa kwa nchi hizo, bali utakuwa na matokeo kinyume na utasababisha kutengwa zaidi kwa nchi hizo tatu kwa kuziondoa katika diplomasia ya baadaye."
-
Mkuu wa Majeshi ya Iran: Marekani, Israel zilishindwa kudhoofisha uwezo wa Iran wa nyuklia, makombora na ulinzi wa anga
Sep 07, 2025 03:07Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesema Marekani na utawala wa Israel zililenga kudhoofisha uwezo wa nyuklia, makombora na ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa vita vya siku 12 mwezi Juni mwaka huu, lakini walishindwa kufikia malengo yao makuu.
-
Araghchi: Iran na IAEA zinakaribia kuunda fremu mpya ya ushirikiano
Sep 06, 2025 23:20Iran imesema imekaribia sana kubuni mfumo mpya wa ushirikiano baina yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), miezi kadhaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii kuipelekea Tehran kusimamisha ushirikiano wake na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Sambamba na kuanza duru mpya ya mazungumzo, Iran yatilia mkazo diplomasia katika kadhia ya nyuklia
Sep 06, 2025 03:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa liidhinishe juhudi za kidiplomasia katika kushughulikia mpango wa nyuklia wa Tehran na kukomesha vitendo vya "kinyume na sheria" vya Ulaya.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa
Sep 05, 2025 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema, mazungumzo yake na viongozi wa Qatar yalikuwa yenye faida na mafanikio makubwa na yalifanyika kwa uzito maalumu na akaongezea kwa kusema: "kwa bahati nzuri, hakuna tofauti zozote kati ya nchi hizi mbili, na sutafahamu iliyojitokeza imetatuliwa kikamilifu na ziara hii".
-
"Hatua ya nchi za Ulaya kuamilisha utaratibu wa snapback ni ya kiholela"
Sep 05, 2025 08:38Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswalia leo hapa Tehran amesema: Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, jaribio lolote la kubadilisha Azimio Nambari 2231 linadhoofisha itibari ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuamilisha utaratibu wa "snapback" wa kurejesha vikwazo vya baraza hilo dhidi ya Iran ni ya kiholela.