-
Iran yakaribisha upatanishi wa Oman uliopelekea US kusitisha mashambulizi dhidi ya Yemen
May 08, 2025 03:36Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei amekaribisha taarifa ya Oman kuhusu kusitishwa kwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen, akisema kuwa nchi za eneo hili hazitasahau Muqawama wa watu wa Yemen dhidi ya uvamizi wa kigeni.
-
Araqchi atahadharisha kuhusu ghadhabu ya Wairani ikiwa Trump atabadlisha jina la Ghuba ya Uajemi
May 07, 2025 23:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametahadharisha kuhusu ghadhabu ya Wairani wote baada ya tetesi kwamba Rais Donald Trump wa Marekani ana mpango wa kubadili jina la Ghuba ya Uajemi katika ziara yake nchini Saudi Arabia, wiki ijayo.
-
Baqaei: Iran ina wasiwasi mkubwa kufuatia kuongezeka mzozo kati ya India na Pakistan
May 07, 2025 22:52Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Tehran ina wasiwasi mkubwa kufuatia kuongezeka mivutano kati ya India na Pakistan na amezitolea wito pande mbili kujizuia kuchukua hatua.
-
Imam Khamenei: Ustaarabu wa Kiislamu ni kinyume cha ustaarabu wa sasa wa kimaada
May 07, 2025 10:35Katika ujumbe wake kwa kongamano la "Miaka 100 wa Kuanzishwa Hauza ya Qum nchini Iran," Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Kazi muhimu zaidi ya Hauza na taasisi ya kielimu ya vyuo vikuu vya kidini, ni kufikisha ujumbe wa wazi na kuweka msingi wa ustaarabu mpya wa Kiislamu."
-
Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yafunguliwa
May 07, 2025 09:34Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yamefunguliwa leo asubuhi katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wakiwemo Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu, Abbas Salehi, na Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf.
-
Jibu la mkato la Iran kwa porojo la Netanyahu
May 07, 2025 05:28Amir-Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la umoja huo kujibu porojo na upayukaji wa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu dhidi ya Iran.
-
Russia na Iran zasisitiza kushirikiana zaidi katika siasa za kigeni
May 07, 2025 03:43Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wamesisitiza juu ya azma ya nchi zao ya kushirikiana zaidi katika uga wa siasa za kigeni.
-
Iran: Tutajibu chokochoko yoyote ya kijeshi ya Marekanii au Israel
May 07, 2025 03:43Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hatua zozote za kijeshi za Marekani au utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mamlaka ya kujitawala na maslahi ya taifa ya Iran zitapatiwa jibu la haraka na mwafaka.
-
Tamasha la Asubuhi: Sauti ya Muqawama dhidi ya ubeberu wa kimataifa, linaendelea Tehran
May 07, 2025 03:07Tamasha la tatu la vyombo vya habari la "Sobh", (Asubuhi) kwa ajili ya kuwaenzi watu mashuhuri wanaopinga ubeberu, kuanzia wabunge wa zamani wa mabunge ya Ulaya na Uingereza hadi mwandishi wa habari wa Palestina kutoka Gaza, linaendelea kupaza sauti ya mapambano na Muqawama dhidi ya ukandamizaji wa kimataifa.
-
Msemaji wa serikali ya Iran: Vikwazo vya Marekani vinalenga maisha ya raia
May 07, 2025 03:04Msemaji wa Serikali ya Iran amesema kuwa vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vinaathiri maisha ya watu wa kawaida.