Larijani: Hizbullah ya Lebanon ni chimbuko la heshima na fahari kwa Uislamu
-
Ali Larijani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran akihutubia nchini Lebanon
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema: "Leo Hizbullah nchini Lebanon ni harakati hai na endelevu inayouletea Uislamu heshima na fahari."
Dlt. Ali Larijani amesema hayo katika hotuba yake kwa wananchi wa Lebanon karibu na kaburi la shahidi Sayyed Hassan Nasrullah mjini Beirut, kuongeza kuwa: "Juhudi za Shahidi Sayyed Hassan Nasrullah za kuimarisha Hizbullah zilikuwa hatua ya kweli na ya kudumu kwa jamii za Kiislamu."
Amesema, "Shahid Sayyed Hassan Nasrullah alikuwa halisi katika fikra za Kiislamu," na kuongeza: "Mengi ya yale yanayotajwa juu yake kwenye vyombo vya habari ni sifa za mapambano yake, lakini mwelekeo mwingine wa mtu huyu wa Mwenyezi Mungu ni fikra halisi ya Kiislamu aliyokuwa nayo."
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran alitaja mielekeo ya kiirfani miongoni mwa sifa nyingine za shahid Sayyed Hassan Nasrullah, na kuongeza: "Mazingira ya zama hayakumuathiri na alikuwa ni mtu aliyejitengeneza mwenyewe."
Kadhalika Larijani amesema kuwa, uasili katika njia ya mapambano katika njia ya Mwenyezi Mungu ni sifa nyingine ya Shahidi Sayyed Hassan Nasrullah, na akaeleza kwamba, “Njia aliyoiweka kwa ajili ya Hizbullah ni njia ambayo ndani yake kuna ukamilifu wa kimapambano ya kiroho na kiakili.
Akivihutubu vikosi vya Hizbullah ya Lebanon amesema: "Iwapo mnataka kufuata njia ya shahidi Sayyed Hassan Nasrullah, wajibu wenu leo ni kudumu katika muqawama. Tumelitangaza hili na tunasema kwamba sisi tuko pamoja nanyi na tunakuungeni mkono daima."