Dkt. Larijani: Muqawama ni rasilimali ya kitaifa ya Lebanon
Dkt. Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, muqawama ni mtaji na rasilimali ya kitaifa la Lebanon.
Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran ambaye yuko safarini nchini Lebanon, leo amekutana na kuufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Joseph Aoun katika mkutano wake wa kwanza wa kidiplomasia mjini Beirut.
Akisisitiza kwamba "Iran haiingilii maamuzi ya Lebanon," Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa amesema: "Hizbullah ni harakati ya asili, muqawama unatawala nyoyo, na hautaangamizwa kwa kutolewa taarifa fulani ya kisheria."
Sambamba na kuelezea kufurahishwa kwake na kuweko kwake nchini Lebanon Larijani amesema: "Nguvu ya Iran inatokana na mshikamano wa kitaifa uliopo nchini Iran. Nguvu ya Iran inahusiana na mapinduzi makubwa ya wananchi. Mapinduzi ya Iran yalikuwa ni miongoni mwa mapinduzi makubwa yaliyopendwa na watu wengi, na kamwe hatuwaangalii marafiki zetu kama chombo. Tunaamini kwamba muqawama una fahamu za kina na fikra pana na hauhitaji mwongozo."

Kuhusu uamuzi wa serikali ya Lebanon wa kuipokonya silaha Hizbullah ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, kufuatia mashinikizo ya Marekani na utawala wa kizayuni, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema: "Nchi za nje ya Lebanon hazipaswi kutoa amri kwa nchi hii."
Aidha amesema, watu wa Lebanon ni taifa lililokomaa na linaweza kufanya maamuzi yao wenyewe, na uamuzi wowote ambao Hezbollah hufanya kwa akili ya kawaida unakubalika kwetu. Serikali ya Lebanon inaweza kufanya maamuzi yake kwa kushauriana na muuqawama.