-
Pezeshkian: Marekani inafanya uporaji mchana kweupe
May 21, 2025 06:41Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa, rais wa Marekani Donal Trump alisema akiwa nchini Saudia kwamba watu wengine wanapora na kuiba wakati mwenyewe Trump ndiye anayefanya wizi na uporaji mchana kweupe na mbele ya macho ya walimwengu.
-
Bunge lapasisha makubaliano ya kimkakati ya Iran na Russia
May 21, 2025 06:40Wajumbe wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wamepasisha rasimu ya Mkataba wa Ushirikiano Kamili wa Kimkakati kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Shirikisho la Russia.
-
Kharrazi: Dunia ya kambi moja imeyoyoma, kuna haja ya mazungumzo ya kikanda
May 21, 2025 04:03Mkuu wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Iran amesisitiza kuwa mfumo wa kambi moja umeyoyoma na sasa kumeibuka madola yenye nguvu ya kikanda na kusema: "Suluhisho pekee la changamoto za Mashariki ya Kati ni mazungumzo ya moja kwa moja kati ya nchi za eneo hilo bila ya uingiliaji wa madola ya nje ya kanda hiyo."
-
Wabunge wa Iran walaani hatua ya Bunge la UK kuitambua IRGC kuwa 'kundi la kigaidi'
May 20, 2025 22:57Wabunge wa Iran wamelaani vikali hatua ya wabunge wa Bunge la Uingereza ya kuliorodhesha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kuwa shirika la kigaidi, wakiapa kuchukua hatua za kisheria za kujibu mapigo.
-
Kiongozi Muadhamu: Hatusubiri idhini ya yeyote katika kurutubisha madini ya urani
May 20, 2025 10:19Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Iran haingojei ruhusa ya mtu yeyote ili kurutubisha madini ya urani na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ina sera zake.
-
Araqchi: Iran imo mbioni kuanzisha tena uhusiano na Bahrain na Misri
May 20, 2025 10:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamahuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mchakato wa kurejesha uhusiano wa nchi hii na Bahrain na Misri umeanza.
-
Ujumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran katika kufafanua upya diplomasia ya kikanda
May 20, 2025 09:31Kikao cha nne cha Jukwaa la Mazungumzo Ya Tehran kimefanyika hapa mjini Tehran, kikisisitiza "wakala wa kikanda" na ulazima wa kuunda utaratibu mpya kutoka ndani ya eneo.
-
Rais Pezeshkian: Hatusubiri maagizo au ruhusa kutoka kwa mtu yeyote
May 20, 2025 03:25Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran kamwe haisubiri maagizo au ruhusa kutoka kwa mtu yeyote na itaendelea kusimama imara kulinda haki zake kwa nguvu zake zote.
-
Jenerali: Maadui watalipa gharama isiyoweza kuelezeka wakihujumu Iran
May 20, 2025 02:57Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Mohammad Hossein Bagheri, ameonya kuwa hatua yoyote ya uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, ikiwemo ukiukaji wa anga ya taifa, itawaletea maadui gharama kubwa isiyoweza kufidiwa.
-
Iran yataka maendeleo ya Akili Mnemba katika nchi za Kiislamu
May 20, 2025 02:56Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad-Reza Aref, ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuwekeza na kuendeleza Akili Mnemba (AI) kwa kuzingatia kanuni kuu tatu za ushirikiano wa pande kadhaa, mshikamano wa kisayansi, na miundombinu ya pamoja.