-
Mkuu wa Kikosi cha Quds: Iran itaendelea kuwa bega kwa bega na Palestina kwa operesheni za kijeshi
Mar 27, 2025 02:58Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko thabiti katika msimamo wake wa kuunga mkono kadhia ya Palestina kupitia uungaji mkono wa moja kwa moja kwa vikosi vya Muqawama na kwa operesheni za kijeshi kama zile za Ahadi ya Kweli.
-
Rais Pezeshkian: Taifa la Iran linapaswa kuonyesha umoja katika Siku ya Kimataifa ya Quds
Mar 27, 2025 00:43Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa wananchi wa Iran kuonyesha umoja na mshikamano wao wakati wa Siku ya Kimataifa ya Quds, akisisitiza kwamba kujitokeza kwa wingi wananchi katika siku hii kutaonyesha msaada usiotetereka wa Jamhuri ya Kiislamu kwa malengo ya ukombozi wa Palestina.
-
Balozi wa Iran akosoa kuenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi
Mar 27, 2025 00:39Ali Bahraini, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, amekosoa kuenea kwa chuki dhidi ya Uislamu au kwa maneno mengine Islamophobia katika nchi za Magharibi
-
Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni Tuko kwenye Ahadi Ewe Quds
Mar 26, 2025 22:53Mkuu wa Kamati Kuu ya Intifadha na Siku ya Kimataifa ya Quds amesema kuwa: Tutaadhimisha Siku ya Quds mwaka huu kwa kaulimbiu ya Tuko kwenye Ahadi Ewe Quds ikiwa ni kumbukumbu ya shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, shahidi Haniyeh na makumi ya mashahidi wa kambi ya Muqawama.
-
'Mauaji makubwa zaidi ya watoto': Iran yalaani mauaji ya Israel na US dhidi ya watoto wa Gaza
Mar 25, 2025 23:59Jamhuri ya Kislamu ya Iran imelaani vikali mauaji ya halaiki ya utawala wa Israel dhidi ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, na kuyataja kuwa ni sehemu ya sera ya iliyopangwa ya mauaji ya kimbari yenye lengo la kufuta utambulisho wa Wapalestina.
-
Iran yazionya nchi jirani: Jihadharini na ufitinishaji na ufarakanishaji wa Marekani
Mar 25, 2025 08:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia tuhuma zilizotolewa na viongozi wa Marekani kuhusiana na kuiwekea mashinikizo Iran na akasema: "inavyotarajiwa, nchi jirani na marafiki zitajihadhari na ufitinishaji na ufarakanishaji unaofanywa na Marekani".
-
Qaarii wa kimataifa wa Iran asoma kisomo cha Qur'ani kwenye mikesha ya Lailatul-Qadr, China
Mar 25, 2025 08:20Kwa ushirikiano wa Ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji wa Guangzhou na Ofisi ya Mwambata wa Utamaduni katika mkuu Beijing, Adnan Momineen, msomaji mashuhuri wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran ameshiriki na kusoma Qur'ani katika ibada za mikesha ya Lailatul-Qadr mjini Guangzhou.
-
Iran: Wakimbizi wa Afghanistan watarejeshwa kwao kwa heshima
Mar 25, 2025 03:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, viongozi wa Iran na Afghanistan wameandaa utaratibu mzuri wa pamoja wa kuwawezesha wakimbizi wa Afghanistan waliopo nchini Iran warejee nchini kwao kwa heshima.
-
Iran: Hakuna mazungumzo yatakayofanyika chini ya mashinikizo, lazima Marekani ibadilishe siasa zake
Mar 25, 2025 02:47Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa haitashiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani chini ya mashinikizo ya 'vikwazo vya juu zaidi' na vitisho.
-
Iran inajiundia asilimia 90 ya zana zake za kivita
Mar 25, 2025 02:35Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Viwanda vya Kieletroniki Iran (IEI) amesema kuwa uwezo wa kijeshi na kiulinzi wa Iran unategemea wataalamu wa ndani ya nchi.