-
Ulinzi wa anga wa Iran 'wazuia na kuzima kwa mafanikio' uchokozi wa Israel
Oct 26, 2024 03:36Kikosi cha ulinzi wa anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimethibitisha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya mashambulio ambayo yamelenga maeneo kadhaa katika mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam, na kusema uchokozi huo umezimwa kwa mafanikio.
-
Majibu ya mifumo ya anga ya Iran ndiyo sababu ya kusikika sauti za miripuko pembeni mwa Tehran
Oct 25, 2024 23:33Duru za kiusalama za Iran zimetangaza kuwa, sauti kubwa za miripuko zilizosikika alfajiri ya leo Jumamosi hapa Tehran zimetokana na majibu ya mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran kupiga silaha zilizorushwa dhidi ya baadhi ya maeneo ya pembeni mwa Tehran.
-
Wakristo wa Armenia nchini Iran: Tuko chini ya Kiongozi Muadhamu katika hali zote
Oct 25, 2024 07:21Kaimu Askofu Mkuu wa Wakristo wa Armenia nchini Iran amesema kuwa, wako chini ya amri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika hali zote.
-
Ayatullah Khatami: Visiwa vitatu ni milki ya Iran, vilikuwa na vitaendelea kuwa hivyo
Oct 25, 2024 07:21Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa, visiwa vitatu vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo ni milki ya Iran, vilikuwa hivyo tangu zamani na vitaendelea daima kuwa hivyo katika siku za usoni.
-
Iran yakosoa vitendo vya kigaidi vya Israel nchini Lebanon
Oct 25, 2024 03:23Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya raia wa Iran mjini Beirut na kuyataja kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala ya Lebanon.
-
Rais wa Iran: Njama za Marekani zitasambaratishwa
Oct 25, 2024 03:14Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Utekelezaji wa yaliyoafikiwa katika mkutano wa BRICS utasambaratisha njama za Marekani na washirika wake.
-
Mikutano ya Pezeshkian katika kikao cha BRICS na sisitizo la Iran la kuzingatiwa mitazamo ya pande kadhaa katika mfumo wa kimataifa
Oct 25, 2024 03:03Pambizoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za BRICS huko katika mji wa Kazan nchini Russia, Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi shiriki ambapo amesisitiza haja ya kuzingatiwa mitazamo ya pande kadhaa katika mfumo wa kimataifa.
-
Imam Khamenei: Hizbullah iko hai na inastawi
Oct 24, 2024 23:59Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amempongeza Sayyed Hashem Safieddine, kiongozi wa ngazi za juu wa Hizbullah aliyeuawa shahidi hivi karibuni katika hujuma ya utawala haramu wa Israel, na kuitaja harakati ya muqawama kuwa "mtetezi shupavu zaidi wa Lebanon na ngao madhubuti zaidi dhidi ya uroho wa utawala wa Kizayuni." Aidha amesisitiza kuwa, Hizbullah iko hai na inastawi.
-
Rais Pezeshkian: BRICS, mfano wa mafanikio wa ushirikiano na kuondokana na hatua za upande mmoja
Oct 24, 2024 23:11Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jumuiya ya BRICS ikiwa na malengo yake makubwa imeweza kuwa kielelezo cha mafanikio cha ushirikiano kati ya nchi katika uga wa kimataifa.
-
Iran: Umoja wa Mataifa umepoteza falsafa ya kuwepo kwake
Oct 24, 2024 23:11Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kiigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Umoja wa Mataifa umo katika hali ya kupoteza falsafa ya kuwepo kwake.