Muhammad Islami: Wazayuni wameulemaza Umoja wa Mataifa
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, kivitendo Wazayuni wameulemaza Umoja wa Mataifa na taasisi hiyo iliyokuwa ikipigania haki za binadamu na uadilifu hivi sasa imepoteza kabisa ufanisi na uutendaji wake.
Muhammad Islami alisema hayo jana, katika hafla ya kuwaenzi mashahidi wa Kimbunga cha Al-Aqswa na mashahidi wa muqawama, ambapo ameashiria kura za ndio za nchi 167 katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya watu wa Palestina kuunda nchi huru huru na kusema: Ni Marekani pekee na nchi nyingine zisizopungua tano zilizopinga kuundwa kwa taifa huru la Palestina.
Aidha ameongeza kuuwa, leo hii idadi hiyohiyo yenye ukomo ina jukumu na nafasi muhimu ya kuamua kuhusiana na masuala ya kimataifa na kura ya nchi nyingi duniani inapuuzwa kivitendo.
Kadhalika amesema, katika hali hiyo, kambi ya haki na ukweli, ambayo daima imesimama kidete dhidi ya mwelekeo huu, ina jukumu lililo wazi; sio tu kwamba harakati za kambi hii hazitasimama, bali itaendelea na njia yake kwa nguvu zaidi na kuwafanya watenda jinai kuwajibika.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema, madola ya kibeberu yanajaribu kuimarisha uchumi wao kwa kuzuia teknolojia za hali ya juu katika nchi zinazoendelea na hivyo kuzuia ukuaji wao wa mataifa hayo.