-
IRGC yazindua kituo kipya cha chini ya ardhi cha makombora ya kruzi ya kuteketeza manowari za mashambulizi
Feb 02, 2025 00:07Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimezindua kituo kipya cha chini ya ardhi katika maeneo ya mwambao wa kusini mwa Iran, kinachohifadhi makombora yaliyo tayari kuteketeza manowari za mashambulizi za adui katika eneo la kimkakati la majini.
-
"Urithi wa Mashahidi wa Brigedi za Qassam utatokomeza saratani ya Israel"
Feb 01, 2025 04:28Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema urithi adhimu wa Mashahidi wa Brigedi za Izzudin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, katika vita dhidi ya Israel utatia nuru kwenye mustakbali wa Muqawama.
-
Rais wa Iran: Sehemu kubwa ya matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu yanasababishwa na kuwa mbali na mafundisho ya Qur'ani
Jan 31, 2025 23:37Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe wake katika hafla ya kumalizika duru ya 41 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an katika mji wa Mash'had hapa nchini kuwa: Sehemu kubwa ya matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu hii leo ni matokeo ya kuwa mbali na mafundisho ya Qur'ani.
-
Iran yaonya: Shambulio dhidi ya vituo vyetu vya nyuklia litasababisha 'vita vitakavyoenea katika eneo'
Jan 31, 2025 23:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ametoa onyo kali kuhusu matokeo mabaya ya kitendo cha uchokozi kinachoweza kufanywa, ambacho kinaweza kuuhusisha utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.
-
Spika wa Baraza la Hamas apongeza mchango wa Iran katika kuwatetea Wapalestina
Jan 31, 2025 23:03Muhammad Ismail Darwish, Mwenyekiti wa Shura ya Hamas, ametoa shukurani kwa msaada na uungaji mkono wa Iran kwa watu wa Palestina, na kusema mchango wa Tehran ni muhimu katika mapambano yanayoendelea dhidi ya utawala wa ghasibu wa Israel.
-
Kuhudhuria kwa mara ya kwanza Iran vikao vya Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia (EAEU) ikiwa mwanachama mtazamaji
Jan 31, 2025 23:00Baada ya Iran kukubaliwa kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia, Eurasian Economic Union (EAEU) mazingira mazuri yatakuwa yameandaliwa kwa ajili ya kustawishwa na kuongezwa kwa kasi mabadilishano ya kibiashara na mashirikiano ya kiuchumi kati ya pande mbili, na kuongezeka manufaa zitakayopata pande zote mbili.
-
Iran yaanza sherehe za Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jan 31, 2025 10:03Raia wa Iran leo wameanza sherehe za Alfajiri Kumi ili kuadhimisha mwaka wa 46 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyouangusha utawala wa kifalme wa Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na kusaidiwa na Marekani.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Mafanikio muhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu ni uzalishaji wa sayansi na elimu
Jan 31, 2025 10:00Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu anakutambua kuzalisha elimu na sayansi kuwa ndio njia ya kupata nguvu na kuwa imara, na mafanikio yenye thamani kubwa zaidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ni uzalishaji wa sayansi na harakati ya kuelekea kwenye kilele cha elimu inaofanywa na vijana mahiri wa Iran.
-
Iran yaiambia EU: Kwanza jifunzeni maana ya 'tishio' na 'amani' ndipo muwatuhumu wengine
Jan 30, 2025 02:21Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeushauri Umoja wa Ulaya kwenda kujifunza kwanza maana ya "tishio" , "amani" na "usalama wa kimataifa" kabla ya kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu kwa madai chapwa ya kutishia usalama wa kimataifa.
-
Salami: IRGC ina 'Akili Mnemba' ya kutumia kwenye operesheni ngumu za kijeshi
Jan 29, 2025 23:18Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kikosi cha wasomi cha jeshi hilo la Iran kimejizatiti kwa teknolojia ya Akili Mnemba ili kutekeleza vyema operesheni nzito na ngumu za kijeshi.